Koweit yasaini mkataba wa ununuzi wa ndege 20 na Boeing

Shirika la Koweit la Alafco linalofadhili miradi ya kukoti na kununua ndege limesaini mkataba wenye dhamani ya dollar bilioni 2.2 wa kununua ndege 20 aina ya B 737-8 Max na shirika la Mareekani la Boeing.

Mkataba huo umesainiwa siku ya pili ya maonyesho ya anga ya 2017 yanaofanyika Dubai.

Mkurugenzi wa mauzo wa Boeing, Ihsane Munir, amesema kuwa ndege zitawasilishwa kwa Koweit kuanzia mwaka 2020.

Mwezi June uliopita, Alfaco ilisainii mkataba na shirika la anga la Koweit wa ununuzi wa ndege 4 za B 777-300 ER wenye dhamani ya dollar bilioni 1.358.

Maonyesho ya anga ya 2017 ya Dubai yalianza jumapili. Ni maonyesho makubwa kuwahi kutokea katika kanda ya Mashariki ya kati. Watu 1200 kutoka nchi 53 wameshiriki katika maonyesho hao ikiwa ni pamoja na nchi kama China, Urusi, na Marekani.

Tagi: Boeing , Koweit

Habari Zinazohusiana