Fuat Oktay: "Uturuki yaanza kupiga hatua katika sekta ya teknolojia"

Makamu wa  rais wa Uturuki Fuat Oktay asema kwamba Uturuki yaanza kupiga hatua katika sekta ya teknolojia

Fuat Oktay: "Uturuki yaanza kupiga hatua katika sekta ya teknolojia"

Fuat Oktay, makamu wa rais wa Uturuki amefahamisha kuwa Uturuki yapiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia .

Hayo makamu wa rais ameyazungumza  baada ya Uturuki  kuonesha kuwa imefanya mabadiliko makubwa  na kupiga hatua katika uundaji wa vifaa vya anga vya kivita.

Sekta ya ulinzi nchini Uturuki  imepiga  hatua kwa kuunda kwa vifaa vipya  vya anga vya kivita.

Uturuki iliandaa maonesho  ya vifaa vya kivita vya anga mjini Istanbul TEKNOFEST kuanzia Alkhamis hadi Jumapili.

Uturuki imeanza kuona matunda ya juhudi ambazo wanasayansi  wamejitolea ili kuakikisha kuwa sekta ya ulinzi Uturuki inakuwa imara.

Makamu wa rais wa Uturuki Fuat Oktay amepongeza  tamasha hilo la TEKNOFEST  na kutoa pongezi kwa wote wale ambao  walitoa mchango wao ili kufaanikisha mradi huo ambao lengo lake ni Uturuki kuwa salama.

Maonesho   ya uwezo wa vifaa vya kivita vilivyoundwa  kwa ajili ya jeshi la Uturuki yaliendelea hadi majira ya usiku.

Maonesho hayo yamefanyika kwa ushirikiano na mchango wa  mashirika makubwa ya teknolojia ya Uturuki  kama Aselsan, Roketsan, Baykar, IGA, TAI na shirika la ndege la  Turkish Airlines.Habari Zinazohusiana