Akaunti ya Twitter ya Al Jazeera yafunguliwa baada ya kusimamishwa

Siku ya Jumamosi akaunti ya Al Jazeera yenye wafuasi milioni 12 ilifungwa kwa muda

Akaunti ya Twitter ya Al Jazeera yafunguliwa baada ya kusimamishwa

Siku ya Jumamosi akaunti ya mtandao wa Twitter ya shirika la habari la Qatar kwa lugha ya Kiarabu ilifungiwa kwa muda .

Akaunti hiyo ya kampuni hiyo ya vyombo vya habari ina wafuatiliaji milioni 12.

Televisheni ya Pan-Arab iliandika ujumbe kwa Twitter uliofahamisha kwamba akaunti hiyo imefungiwa kwa muda kwa kuwa na mipango ya kufanya kampeni.

Baadaye ujumbe wa akaunti ya Al Jazeera ukafahamisha tena kwamba imefunguliwa .

Qatar imekumbwa na mzozo dhidi ya ke na mataifa kadhaa ya ghuba yanayodai kuwa inahusika na kuunga mkono ugaidi.

Qatar nayo imekataa shutuma hizo huku ikisema hatua ya mataifa ya kiarabu kujitenga naye kidiplomasia ni hatua isiyo ya haki.

Saudi Arabia,Milki za Kiarabu pamoja na Jordan wamefunga ofisi za shirika la habari la Al Jazeera kufuatia mzozo wa Qatar .Habari Zinazohusiana