Utalii Uturuki : Makao ya watawa  ya Sümela

Utalii Uturuki : Makao ya watawa  ya Sümela

Utalii Uturuki : Makao ya watawa  ya Sümela

 

Makao ya watawa ya Sümela yanapatikana katika aeneo la milima ya  inayoaptikana pambazoni mwa bahari Nyeusi. Ni eneo zuri ambalo linavutia kwa manzara yake.

Eno ambalo kuna patikana makao hayo  ni kati mlima wa Karadağ.  Makao hayo ya watawa ya Sümela linakadiriwa kuwa na urmi wa zaidi ya  miaka 1700 na miongoni mwa makao ya watawa ambayo  yana miaka mingi ulimwenguni.

 Kulingana na taarifa ambazo  zinafahamika kuhusu makao hayo, Sümela ilianzishwa katika karne ya 3 katika kipindi cha utawala wa  Ufalme wa Byzanti. Na historia inafahamisha kuwa viongozi wawili  kutoka Athens ndio waliokuwa wakiongoza.

Umuhimu wa eneo hilo uliendelea kunekana pindi miaka inavyosonga mbele.  Eneo hilo lilizidi  kuwa na umuhimu na kuimarika kwa mara nyingine  katika karne ya 13.

 Katika kipindi cha utawala wa Uthamania Mashariki mwa fukwe za bahari  Nyeusi,  wafalme  walitoa  ulinzi na haki kwa  viongozi ha ona makao yao ya watawa wa Sümela kama ulivyofanya kwa  makao mengine yaliokuwa yakipatikana katika   ardhi yake wakati wa uawala wake.

Ukarabati  ulifanyika    karne ya 18 , kuta ambazo zilikuwa  katika hali iisiokuwa ya kuridhisha, wataalamu walifanya ukarabati .  Jengo refu lilifanyiwa pia ukarabati katika karne ya 19 na kuzidi kuwa na madhara ya kuvutia .

Makao hayo  yalikaliwa na warusi kwa muda ya maiaka miwili tangu mwaka 1916 na kuondoka moja kwa moja mwaka 1923.

Kwa muda wa miaka mingi  makazi hayo ya watawa wa Sümela  yalikuwa yakitumi kwa kutoa mafunzo kwa  makuhani.

 Katika makazi hayo kulikuwa kukipatikana kanisa, vyumba vya mafunzo,  vyumba vya masomo , maktaban a  kisima ambacho kulikuwa kikiaminiwa kuwa kştakatifu. Kuta za makaazi hayo zimewekwa mapambo ya picha ambazo zilichorwa na wachotraji mashuhuri katika historia. Picha hizo zinaonesha maisha  yaliosimuliwa katika Biblia ikiwemo pia  maisha na nabii Issa na B Mariam.

 Makazi hayo ya watawa ayibatizwa pia jina la  Bi Bikira Maria. Enoe hilo linapatikana  kati ya eneo la Maçka na Trabzon.

Ibada ya misa  iliongozwa na kiongozi wa Orthodox   kutoka Ugiriki  Fener  katika makazi hayo ya watawa wa Sümela ilifanyika mwaka  2010.

Kima mwaka, hususan katika msimu wa kiangazi watalii  hutembelea eneo hilo kwa wingi. Ni eneo muhimu miongoni mwa maeneo muhimu kwa wakristo.

Kwa wot wale wanaotaka kutembelea eno hilo , wanaweza pia kutembelea eneo  kunakaopatikana  karsi  na jumba la  ukumbusho la st-Sophia Trabzon na  Atatürk.Habari Zinazohusiana