Uturuki na Utalii, mji wa kihistoria wa Efeso

Uturuki na Utalii, mji wa kihistoria wa Efeso

Uturuki na Utalii, mji wa kihistoria wa Efeso

Kama tunavofahamu  kuwa  katika ardhi ya Anatolia , kuna miji ya kihistoria kutokana na utajiri wake wa kihistoria kwa miaka mingi ya uastaarabu.

Mji wa Efeso ni moja ya miji ya kihistoria.

Eneo la Magharibi mwa Uturuki, mkoa wa Izmir ambapo kunapatika mji wa Efeso, katika kipindi cha  utawala wa Helena, warumi, warumi wa Mashariki ni vipindi tofauti ambavyo vinafahamika katika historia kwa miaka mingi na baadae kufuatiwa na utawala wa Uthmania.

Mji huo ulikuwa na umuhimu kutokana na uwepo wake katika fukwe, mji huo ulikuwa na bandari ambayo ilikuwa ikitegemewa  kitamaduni na biashara katika vipindi tofauti.

Mji huo unaonekana kuwa na umuhimu katika mkubwa katika historia ya Uturuki na Mashariki ya Kati.

Wanahistoria baada ya uchnguzi na utafiti walifahamisha kuwa mji wa Efes ulianza miaka zaidi ya  6000 katika kipindi  ”                Neolithyc” au kipindi cha mawe .

Eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na  wa Hititi ambao walikuwa wakaazi wake katika kipindi hicho.

Katika kipindi cha warumi , Efeso ilikuwa bandari kubwa katika mataifa na tawala zote zilizokuwa barani Asia.

Waturuki waliteka mji huo miaka ya 1330 na kuwa miongoni mwa miji muhimu ya Uturuki katika historia yake. Baada ya muda kupita  mji huo ulikuwa ukipoteza  thamani yake na hata  ukubwa uliokuwa nao. 

Licha ya kupoteza thamani yake hiyo  katika    nyakati tofauti, mji wa Efeso umekuwa kivutia kikubwa cha watalii.

Kila mwaka watalii kutoka katika pembe nne za dunia hutembelea Efeso kama eneo la Selçuk  mkoani İzmir.

Baada ya Efeso kuondolewa  katika  tawala tofauti  katika historia yake , mji wake  una mabaki ya kihistoria ambayo huwavutia watalii hadi leo.

Hatarkati za kuukarabati mji huo wa kihistoria   hufanyika kila mwaka.

 Efeso ni mfano wa kuigwa katika kukua kwa miji, wahandisi katika nyakati tofauti ndio walioujenga mji huo.

Kunapatika jumba la Artemis,  jumba ambalo pia limeorodheshwa  katika mirathi ya dunia.  Vile vile katika historia yake, inatajwa kuwa Yohana aliandika  Ufunua wa Yahya Efeso na inatajwa kuwa Bi Mariam alifariki hapo.

Leo, nyumba alipokuwa akiishi Bi Mariam hutembelea na wakristo na kunapatikana kanila ambalo lilipewa jina lake.


Tagi: Izmir , Uturuki , Efeso

Habari Zinazohusiana