Mapishi ya Kituruki

Jinsi biringanya inavyopikwa nchini Uturuki

Mapishi ya Kituruki

Mojawapo ya mboga inayotumika kwa sana nchini Uturuki ni “Biringanya”.

Mboga hii imechukua nafasi kubwa katika mapishi a Kituruki licha ya kuwa asili yake ni India na ilianza kutumiwa na waturuki baadaye kabisa.

Kuna mapishi mbalimbali ya biringanya nchini Uturuki.

Unaweza ukazioka,ukazichanganya na nyama au bila nyama,unaweza ukazila zikiwa za moto au baridi na unaweza ukazipika kwa kuchanganya na viuongo vingine mbalimbali.

 

Leo tutatizama mapishi ya biringanya ambayo waturuki huita “Karnıyarık” yani “Rivenbelly”.Tunaweza kutafsiri kwa kiswahili kama biringanya iliyokatwa au kupasuliwa.

Mahitaji;

-Biringanya ndogo 6

-Gramu 200 za nyama iliyosagwa

-Nyanya 3

-Pilipili ndefu 6

-Kitunguu saum 1

-Kijiko kimoja cha nyanya ya kuşağa (kijiko cha chakula)

-Nusu glasi ya mafuta

-chumvi ,pilipili manga,pilipili hoho nyekundu.

 

-Menya biringanya zako kuanzia kileleni kwenda juu na kisha weka kwenye maji ya chumvi kwa nusu saa ili kuzuia mafuta.Ondoa kutoka kwenye maji, safisha vizuri ,kausha na kisha kaanga katika mafuta.

 

-Baada ya biringanya kupoa zichanganye na vitunguu maji na saumu katika sufuria na weka katika moto kama unazichoma.Ongeza nyama ya kusaga na koroga mpaka nyama itakapobadilika rangi.Kisha ongeza nyanya,chumvi na viuongo.Subiri kwa dakika 10 na hakikisha mchanganyiko wako hauna maji.

 

-Chukua biringanya nyingine na uzikate katikati.Kisha jaza mchanganyiko wako katikati.Menya nyanya na pilipili hoho kisha uweke juu yake.

 

-Katika bakuli jingine,changanya nyanya ya kopo kwenye nusu glasi ya maji mwaga mchanganyiko wako juu ya bilinganya.

-Weka katika tanuri kwa dakika 20-25. (Nyuzi joto 170).

Chakula chako kiko tayari kwa ajili ya kuliwa.

 Habari Zinazohusiana