Mapishi ya Kituruki

supu ya mtindi

Mapishi ya Kituruki

Maziwa ya mgando au “mtindi” ni maziwa ambayo hutumiwa kwa namna tofauti katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.Baadhi huyanywa kama yalivyo,wengine hutia sukari na ladha nyingine ndani ya maziwa hayo kulingana na utamaduni wa jamii fulani.Je wajua ya kwamba maziwa ya mgando yalianzishwa na waturuki?. Hata neno “YOGHURT” limetoka katika lugha ya kituruki “YOĞURT” ikiashiria maziwa mgando na neno hilo hutumiwa katika lugha nyingi.Maziwa hayo yamekuwa yakitumiwa kama kinywaji toka karne ya 19.Waturuki huyanywa maziwa hayo kama yalivyo,huchanganya na sukari au ladha nyingine tamu,hutumiwa kama mchuzi,au huchanganya na maji na kutumiwa kama kinwaji au supu.

Leo tutatizama jinsi waturuki wanavyotengeneza “supu ya maziwa ya mgando”.

Supu hiyo ijulikanayo kwa jina la “Yayla Çorba” hutengenezwa kama ifuatavyo;

-Glasi 6 za maji au supu ya nyama

-Vijiko viwili vya mchele (kijiko cha chakula)

-Vijiko viwili vya unga (kijiko cha chakula)

-Yai moja

-Glasi mbili za mtindi

-Vijiko viwili vya chumvi na majani ya nanaa yaliyokaushwa (kijiko cha chai)

-Vijiko viwili vya siagi  (kijiko cha chakula).

 

Katika maandalizi; kwanza unaweka maji katika sufuria na kuchemsha. Baada ya kuongeza chumvi ndani ya maji ya moto, ongeza mchele uliyooshwa na changanya mpaka pale mchele utakapolainika. Katika bakuli lingine, changanya yai , unga na mtindi. Ongeza glasi moja ya maji katika mchanganyiko. Ongeza moto katika mchele wako na kisha mimina mchanganyiko wako huku ukiendelea kukoroga polepole .Vikianza kuchemka subiri kwa dakika kumi na kisha zima jiko.Chukua sufuria dogo na uchemshe siagi yako na kuchanganya kidogo na majani ya nanaa yaliyokaushwa kisha subiri kwa sekunde 30.Mwaga siagi yako juu ya supu yako .Ukipenda unaweza kuongeza na pilipili kidogo.

Supu ipo tayari kwa kunywewa.Habari Zinazohusiana