Kevin Hart kusherehesha tuzo za Oscars

Mchekeshaji na mcheza filamu maarufu wa Marekani Kevin Hart kuwa mshereheshaji wa tuzo za Oscars za 91 zitazofanyika mapema Mwakani

Kevin Hart kusherehesha tuzo za Oscars

Kevin Hart mcheza filamu na mchekeshaji maarufu kutoka Marekani ameteuliwa kuwa mshereheshaji wa tuzo za Oscars msimu wa  91, zitazofanyika Los Angeles nchini Marekani Februari 24, 2019.

Hart, ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Intagram amesema ndoto yake ya muda mrefu ya kuwa mshereheshaji wa tuzo za Oscars imetimia.

Katika ukurasa wa twitter wa waandaaji wa tuzo hizo, Akademia ya elimu na sanaa ya filamu ya Amerika wamemtangaza Hart kwa furaha wameandika " Tunawatangazia kujiunga kwa Hart katika familia".

Hart alipata umaarufu zaidi katika filamu kupitia filamu zake kama "Ride along","Jumanji: Welcome to the jungle", na "Night school"

 

 

 Habari Zinazohusiana