Trump azikejeli tuzo za Oscar

Rais Donald Trump amezungumza kuhusu tuzo za Oscars zilizofanyika siku ya Jumapili.

Trump azikejeli tuzo za Oscar

Rais Donald Trump amezungumza kuhusu tuzo za Oscars zilizofanyika siku ya Jumapili.

Tuzo hizo ambazo zinasemekana kutizamwa na watu wachache zimekejeliwa na Trump.

Trump amesema kuwa tatizo kubwa la tuzo hizo ni kwamba hakuna nyota yoyote aliyekuwa katika sherehe hizo,na hiyo ndio sababu kuu ya watu kutozitizama.

Trump akiendelea kuzungumza kuhusu tuzo za Oscar zilizotizamwa na watu wachache katika historia amesema kuwa tatizo ni  kwamba hakuna nyota aliyebaki isipokuwa yeye.

Hata hivyo mwishoni Trump aliandika kuwa alikuwa anatania tu.

Donald Trump ameandika ujumbe huo kuhusu hafla ya 90 ya tuzo za Oscar katika mitandao ya kijamii.

Sherehe hizo zilizofanyika siku ya Jumapili zinasemekana kutizamwa na watu milioni 26.5 ikiwa ni idadi ndogo kabisa katika miaka ya hivi karibuni.Habari Zinazohusiana