Hikaya za Anatolia

Leo katika hikaya za Anatolia tutatizama kisa cha mchungaji wa wanyama katika milima ya Aegean

Hikaya za Anatolia

Leo katika hikaya za Anatolia tutatizama kisa cha mchungaji wa wanyama katika milima ya Aegean.Kutokana na mabadiliko katika hali ya hewa na misimu mchungaji huyo wa kondoo alikuwa akiwahamisha wanyama wake kutoka sehemu moja kuelekea sehemu nyingine.

Siku moja ilikuwa imefika wakati wa joto na mchungaji huyo alilazimika kuhama na kondoo wake na kuelekea sehemu nyingine akiwatafutia lishe pamoja na maji  ya kunywa.Mara mchungaji wa kondoo akapitiwa na usingizi.Kondoo walikuwa wakinywa maji na kula kama ilivyokuwa kawaida.Basi walitokea wezi kadhaa wakataka kuiba kondoo wale.Wezi hao walijaribu kuwachukua kondoo wale lakini hakuna kondoo hata mmoja aliyekuwa akisogea.

Mchungaji aliamka na kukuta kuwa  kondoo wake wanataka kuibiwa.Aliwashangaa na akabaki amewatizama jinsi walivyokuwa wakihangaika.Wezi wale walipoona mchungaji ameamka waliamua kumfunga mikono na kumteka nyara.Lakini bado hakuna kondoo hata mmoja alisogea hata kwa hatua moja.

Wezi wale waliamua kumuuliza mchungaji yule kuwa ni vipi kondoo wale hawafanyiharakati za aina yoyote?. Mchungaji akawaambia kuwa kwanza nifungueni mikono na miguu yangu ili niweze kuwasaidia kuwatembeza kondoo hao.Alipofunguliwa mikono alichukua filimbi yake na kuanza kupiga muziki mzuri sana.

Kondoo kweli walianza kutembea baada ya kusikia mlio wa filimbi.Wezi walidhani wamepata kumbe wamepatikana maana kijiji kizima kiliposikia mlio ule kilijua moja kwa moja kuwa kuna mchungaji anataka kuibiwa wanyama wake.Hili lilikuwa ndio dhumuni kubwa la mchungaji yule kupiga filimbi.

Walikuja wanakijiji na kuwakamata wezi wale.

Wakati kijana yule alipopiga filimbi ile mtu wa kwanza kuisikia alikuwa ni binti wa kiongozi wa mahala hapo.Aliisikia sauti ile na kujua maana yake.Bila kupoteza muda aliwaarifu wanakijiji wenye silaha na hivyo ndivyo wezi  walivyokamatwa.Baada ya tukio hilo kiongozi wa kijiji hicho alitambua kuwa huenda binti yake alimpenda mchungaji yule.Alipata wasiwasi kwani katika zama hizo ilikuwa sio rahisi kwa mtu maskini kama mchungaji kupewa binti wa mfalme.

Mfalme alimuita mchungaji yule na kumuambia kuwa anampa masharti na endapo atayatimiza basi ataweza kumuozesha na binti yake.Alimuambia kuwa endapo ataweza kuwazuia kondoo wake kunywa maji baada ya kukaa kiu kwa muda wa siku tatu basi sharti litakuwa limekamilika.Mchungaji alikubali na kondoo wakakalishwa bila maji na kulishwa chumvi kwa muda wa siku tatu.

Baadae walivutwa mpaka karibu na mkondo wa maji na kisha mchungaji akaanza kupiga filimbi yake.Kondoo wale walikuwa wakipita maji yale bila kunywa wakifuata sauti ya mchungaji wao.Wote walipita isipokuwa kondoo mmoja.Kondoo huyo alikuwa akifuata maji na kusimama baadae alikuwa akirudi kwa mchungaji wake akifuata sauti ya filimbi ile.Kijiji kizima kilikuwa kikitizama jinsi mchungajia livyokuwa akiweza kuwalinda na kuwaamrisha kondoo wake kwa kutumia filimbi.Baada ya muda mfupi kondoo mmoja alikufa kutokana na kiu na hivyo ndivyo mfalme yule alipoguswa na kuamua kutimiza ahadi yake ya kumuozesha binti yake kwa mchungaji wa kondoo.

Tukutane tena juma lijalo kwa hikaya motomoto za Anatolia.Habari Zinazohusiana