Dembele kutoshuka dimbani kwa siku 15

Mshambuliaji wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele kutoshuka dimbani kwa siku 15, ifahamu sababu

Dembele kutoshuka dimbani kwa siku 15

Mshambuliaji wa Ufaransa anayechezea timu ya soka ya ligi kuu ya Uhispania ijulikanayo kama La liga, Ousmane Dembele kutushuka dimbani kwa siku 15 kutokana na majeraha.

Dembele ,21,alipata majeraha hayo wakati wa mchezo baina ya Barcelona na Leganes ambapo Barcelona iliibuka na ushindi wa bao 3-1. Katika mchezo huo imethibika kwamba aliteguka fundo la mguu wa kushoto.

Dembele atarudi uwanjani baada ya siku 15. Katika michezo 27 ya msimu huu aliyoingia dimbani Dembele amefanikiwa kutupia magoli 13 nyavuni.


Tagi: Dembele

Habari Zinazohusiana