Licha ya kutumbuliwa Madrid yatinga robo fainali

Real Madrid yatumbuliwa na Leganes kombe la Mfalme wa Uhispania, yabahatika kutinga robo fainali

Licha ya kutumbuliwa Madrid yatinga robo fainali

Wiki ya 16 ya kombe la Mfalme limeendelea kwa michezo mbalimbali, mmoja wapo ukiwa ni baina ya Real Madrid na Leganes, ambapo Real walishindwa kufurukuta kwa kufungwa goli 1-0.

Licha ya Real Madrid kupoteza mchezo huo imefanikiwa kutinga robo fainali kutokana na kwamba mchezo wakwanza baina ya timu hizo Madrid walishinda goli 3-0.

Goli la Leganes lilipatikana dk ya 31 kupitia kwa mchezaji wao Martin Braithwaite.

Kocha wa Leganes alionyeshwa kadi nyekundu na kulazimika kutoka nje ya uwanja mnamo dk 86 kutokana na kugomea maamuzi ya mwamuzi.

 Habari Zinazohusiana