Timu ya Monaco yamsaini kiungo kutoka Chelsea

Timu ya Ufaransa imetangaza ujio wa Fabregas kutoka Chelsea katika mkataba utakaodumu hadi mwezi Juni mwaka 2022

Timu ya Monaco yamsaini kiungo kutoka Chelsea

 

Timu ya mpira ya mpira wa miguu ya Ufaransa imemsaini kiungo kutoka Chelsea ambaye ni raia wa Uhispania Cesc Fabregas siku ya Ijumaa.

Ukurasa wa mtandao wa Twitter wa timu hiyo uliandikwa kwamba timu ya  AS Monaco ina furaha kubwa kutangaza ujio Cesc Fabregas  kutoka timu ya Chelsea FC katika mkataba utaodumu hadi Juni 2022.

 Fabregas ,31, alithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii kwa kusema kwamba ni heshima kubwa kwake kuanza safari yake mpya katika timu yenye historia kubwa. Monaco kutakuwa nyumbani kwake kwa kipindi cha miaka 3.5 na kwamba anasubiri kwa hamu kubwa kukabiliana na changamoto hiyo mpya.Habari Zinazohusiana