Barcelona washindwa kutamba mbele ya Levante

Yachapwa goli 2 kwa 1 katika mchezo wa kombe la Mfalme.

Barcelona washindwa kutamba mbele ya Levante

 

Barcelona yashindwa kutamba mbele ya Levante, baada ya kufungwa goli  2-1 katika mchezo wa kombe la mfalme.

Nyota wa barcelona kama Lionel Messi, Luis Suarez, Gerard Pique, Ivan Rakitiç na Jordi Alba hawakushiriki katika mchezo huo.

Levante ambao ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huo walipata magoli yao kupitia Erick Cabaco (Dk. 4) na Borja Mayoral (Dk. 18) huku goli la Barcelona likipatikana kwa mkwaju wa penati dakika ya 85. Penati ilipigwa na Philippe Coutinho.

 Habari Zinazohusiana