Salah atwaa tuzo ya mchezaji bora wa CAF mwaka 2018

Mohamed Salah atangazwa kuwa mwanasoka bora wa shirikisho la soka barani Afrika CAF

Salah atwaa tuzo ya mchezaji bora wa CAF mwaka 2018

 

Mchezaji Nyota wa timu ya Liverpool, mwenye asili ya Misri Mohamed Sallah atawazwa kuwa mchezaji bora  wa mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa mwaka 2018 - hii ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo.

Salah, 26, alimshinda mwenzake wa Liverpool Sadio Mane kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang.

Alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika nchini Senegal Jumanne.

"Nimekuwa na ndoto ya kushinda tuzo hii tangu nilipokuwa mdogo na sasa nimefanya hivyo mara mbili mtawalia," Salah alisema.

11 ya kwanza bora kwa mwaka 2018 ni kama ifuatavyo:

 Denis Onyango (Mamelodi Sundowns/Uganda), Serge Aurier (Tottenham/Ivory Coast), Medhi Benatia (Juventus/Morocco), Eric Bailly (Manchester United/Ivory Coast), Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal); Naby Keita (Liverpool/Guinea), Thomas Partey (Atletico Madrid/Ghana), Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria); Mohamed Salah (Liverpool/Misri), Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/Gabon), Sadio Mane (Liverpool/Senegal)

 


Tagi: Salah

Habari Zinazohusiana