Mayweather audhihirishia ulimwengu kuwa yeye ndio mbabe wa ndondi

Amtangwa Teshin Nasukawa ndani ya dakika 2 na kuondoka na kitita cha dola milioni 9 kama zawadi ya ushindi

2018-12-31T160811Z_999784759_RC1DA7B2A640_RTRMADP_3_BOXING-JAPAN-MAYWEATHER.JPG

 

Mbabe wa mchezo wa ndondi kutoka Marekani ambaye hajawahishindwa Floyd Mayweather, aendeleza ubabe kwa kumtwangwa Tenshin Nasukawa mcheza mpiganaji wa kickbox kutoka Japan. Kwa ushindi huo Mayweather ameondoka na kitita cha dola za kimarekani milioni 9 kama zawadi ya ushindi. 

Mayweather alifanikiwa kumtwanga Nashikawa kwa Knockout ndani ya dakika mbili.

Mchezo huo ulifanyika mji mkuu wa Japan Tokyo katika kilele cha sherehe za mwaka mpya. Mayweather alimpiga mpinzani wake huyo mwenye umri wa miaka 20 kirahisi, na mara zote tangu kuanza kwa mpambano alionekana akitabasamu. 

Rekodi ya Mayweather imezidi kuwa nzuri kwani sasa anakuwa ameshinda michezo yake yote 51 katika ndondi za kulipwa bila kupigwa hata mmoja.

 Habari Zinazohusiana