Iniesta ashiriki filamu ya kulitangaza jiji la Kobe

Andres Iniesta ashiriki filamu ya kulitangaza jiji la Kobe la nchini Japani

Iniesta ashiriki filamu ya kulitangaza jiji la Kobe

Mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania anayechezea klabu ya Vissel Kobe ya Japani, Andres Iniesta ameshiriki katika kuimarisha mawasiliano baina mji wake anapotokea,Barcelona na jiji la Kobe nchini Japani.

Iniesta alishiriki katika filamu ya kulitangaza jiji la Kobe,  iliyoandaliwa na jiji hilo kusheherekea miaka 25 ya ushirikiano baina ya jiji la Kobe na Barcelona.

Katika filamu hiyo Iniesta anasikika akisema, "Katika mji huu mzuri uliojawa vivutio vya asili unaweza onja ladha maridhawa kabisa, mimi na familia yangu tunaioenda sana Kobe".

Iniesta mwenye umri wa miaka 34 ameshinda magoli mawili katika michezo 11 ya ligi y Japani aliyoshiriki na timu yake ya Vissel Kobe. Timu hiyo ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo na ina alama nne juu ya mstari wa kushuka daraja.

 

 

 Habari Zinazohusiana