Serena Williams  atozwa faini ya Dola  17 000

Serena Williams atozwa faini ya dola 17 000  kufuatia matukio ya  katika  fainali ya Tennis Marekani

Serena Williams  atozwa faini ya Dola  17 000

Mchezaji nyota wa  kimataifa wa Tennis wa kike wa Marekani Serena Williams ametozwa faini ya dola  17 000 baada ya  mechi ya fainali iliochezwa baina yake na Naomi Osaka .

Katika mechi hiyo Serena Williams alionekana mwenye ghadhabu dhidi ya  muongozi ambae alituhumiwa  kuwa na upendeleo katika maamuzi yake.

Serena Williams amemuomba  muongozaji huyo  kuwa muadilifu  wakati wa kutoa adhabu kwa makosa  katika mchezo.

Muamuzi huyo kwa jina la  Carlos Ramos ametuhumiwa na Serena kutokuwa na uadilifu jambo ambalo limepelekea  mchezaji huyo kutozwa faini ya dola 17 000.

Serena William alipewa adhabu kama hiyo mwaka 2009 na mwaka 2011.Habari Zinazohusiana