Wafahamu wagombea wa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA  mwaka 2018

Shirika la kabumbu la kimataifa la FIFA limetoa orodha ya majina matatu ya wachezaji watakaogombea  tuzo ya mchezaji bora wa FIFA 2018

Wafahamu wagombea wa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA  mwaka 2018


Shirikisho la kabumbu la kimataifa  FIFA limetangaza majina ya wacheza kabumbu ambao watagombea tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mwaka 2018.

Miongoni mwa wachezaji waliokuwa wameorodheshwa kugombea tuzo hiyo, wachezaji watatu pekee ndio ambao wamesalia katika kinyanganyiro hicho.

Kutoka  timu ya   Real Madrid Modric, kutoka katika timu ya Juventus Ronald na Moh Salah wa Liverpool wanagombea tuzo hiyo ya mchezaji bora wa FIFA  mwaka 2018.

Ifahamike kuwa hakuna mchezaji yeyote kutoka katika  timu ya taifa ya Ufaransa alieorodheshwa  kugombea tuzo hiyo  licha ya kushinda kombe la dunia la FIFA  mwaka 2018  nchini Urusi.

Washindi watatangazwa Septemba 24 mjini London nchini Uingereza.Habari Zinazohusiana