Juve kuivaa Man United, Tottenham kundi la kifo UCL

Juve kuivaa Man United, Tottenham kundi la kifo UCL

Juve kuivaa  Man United, Tottenham kundi la kifo  UCL

Droo iliyosubiriwa kwa hamu  ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu wa 2018/19 imetangazwa hii Leo na kubainisha nafasi za vilabu 32 barani Ulaya. 

Klabu ya Juventus  imejikuta uso kwa uso na mashetani wekundu na kuangukia kundi moja. Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United, Christiano Ronaldo atakua kibaruani kupambana na mabosi wake hao wa zamani ambapo kwa sasa yeye anaitumikia klabu ya Juventus. 

Nao Tottenham wamejikuta wakidondokea katika kundi gumu kabisa wakitoana meno na Barcelona ya nchini Hispania, Internationale ya Italia pamoja na PSV. 

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza, Manchester city wamedondoka katika kundi jepesi kuliko yote na hivyo kufanya njia yao kuwa mteremko. 

Liverpool wao watakua kundi moja na timu za PSG ya Ufaransa, Napoli ya Italia na Crevna Zevzda. 

Bingwa mtetezi wa Mashindano haya, Real Madrid atakua kibaruani kuchuana na AS Roma pamoja na CSKA Moscow. 

Mtanange wa mashindano hayo unatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi Septemba.Habari Zinazohusiana