Kibarua cha Mourinho matatani Manchester United

Kibarua cha Mourinho matatani Manchester United

Kibarua cha Mourinho matatani Manchester United

 


Kocha mkuu wa mashetani wekundu, Manchester United amejikuta katika wakati mgumu baada ya timu yake kuanza vibaya ligi kuu. 


Mpaka sasa Manchester United imeshacheza michezo mitatu na imepoteza miwili kati ya hiyo, matokeo ambayo yanaiweka timu hiyo Katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi. 


Inasadikika kuwa Mourinho amekua na msuguano na baadhi ya wachezaji kama Mfaransa Paul Pogba, jambo ambalo linaondoa umoja klabuni hapo. 


Endapo Mreno huyo atapoteza mchezo wake unaofuata wa tarehe 1 Septemba, atakua hatarini na hata kuondoka katika klabu hiyo. 


Wataalam wa mambo wanawataja makocha kama Zinedine Zidane na Pochettino kuwa na uwezekano mkubwa wa kurithi mikoba hiyo endapo tu Mou atafungasha vilago. 
Ikumbukwe kuwa Mzee Jose alijiunga na klabu hiyo msimu wa 2016 na kufanikiwa kutwaa mataji kadhaa likiwemo lile la Europa league. Lakini msimu uliopita mambo hayakuashwari ambapo mashetani wekundu waliambulia patupu na kukosa hata kombe la kuku.Habari Zinazohusiana