Tottenham yainyuka Man United tatu mzuka

Timu ya soka ya Manchester United ilijikuta ikikubali kipigo cha goli tatu kwa Tottenham Hotspurs.

2018-08-27T200655Z_395624553_RC1461110130_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-TOT.JPG
2018-08-27T210621Z_1401866178_RC182B080DF0_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-TOT.JPG
2018-08-27T202314Z_1876397250_RC1E5C8E2440_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-TOT.JPG
2018-08-27T210437Z_1039308687_RC19B4C1A4F0_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-TOT.JPG
cats.jpg


Timu ya soka ya Manchester United ilijikuta ikikubali kipigo cha goli tatu kwa Tottenham Hotspurs. 


Miamba hiyo ya London ilijitutumua na kumaliza uteja wake kwa United wakiwa Old Trafford. Ilizoeleka kuiona Tottenham ikiloana magoli pindi ifikapo Old Trafford. 
Ingawa Mechi ilianza kwa kasi ya nguvu huku kila mmoja akiliwania lango la mwenzie, kipindi cha kwanza kiliisha kwa matokeo kuwa 0-0. 


Mapema kipindi cha pili, Harry Kane alianza kuwalowesha mashetani hao wekundu katika dakika ya 50 ya mchezo, kabla ya Lucas Moura kutupia msumari wa pili dakika mbili Mbele. Hali iliendelea kuwa tete kwa upande wa vijana wa Mourinho ambao walionekana kuzidiwa kimchezo na wakakubali goli la 3 dakika za mwishoni. 


Msimu huu haujaanza vizuri kwa upande wa Man U ambao katika mechi tatu za kwanza wamejikuta wakigawa point 6.Habari Zinazohusiana