Merkel azungumzia mjadala uliomuhusu Mesut Özil

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel azungumzia kuhusu mjadala uliomuhusu nyota wa kabumbu  mwenye asili ya Uturuki

Merkel azungumzia mjadala uliomuhusu Mesut Özil

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel asema kuwa hakuridhishwa na mjadala uliomuhusu nyota wa kabumbu wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki Mesut Özil.

Merkel amesema kuwa iwapo mtu yeyote  ambae ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya kigeni  atakuwa  hajatendewa haki katika jamii, jambo hilo linatakiwa kuchukuliwa na umuhimu  na kuzungumziwa.

Merkel amesema kuwa hkufurahishwa na mjdala uliomzungumzia Özil  ambea alitangaza rasmi kuacha kuchezea timu ya taifa ya Ujerumani kutokana na tuhuma za kibaguzi.

Kituo cha runinga cha ARD kimemuhoji Angela Merkel mabae amekumbusha  kuwa  rais Frank-Walter  Steinmeier alikemea ubaguzi wakati alipoandaa kahawa na wahamiaji na kusisitiza kuwa hakuna utofauti wowote kati ya raia wa Ujerumani.Habari Zinazohusiana