Barcelona yatwaa Super cup

Barcelona yatwaa Super cup

Barcelona yatwaa Super cup

Mchezo mkali na wa kusisimua ulichezwa hapo Jana Baina ya mabingwa wa ligi kuu ya Hispania,Barcelona na Sevilla kuwania kombe la Super cup. 

Mechi hiyo iliyochezwa nchini Morocco ilihudhuriwa na mashabiki kemkem  wa soka, mechi ambayo iliashiria kufunguliwa kwa msimu mpya wa La Liga. 

Barcelona iliibuka bingwa wa mchezo huo kwa kuichabanga Sevilla Magoli mawili kwa Moja. 

Sevilla ilikua ya kwanza kupata goli mwanzoni kwa mchezo huo, lakini Barcelona ilifanikiwa kurudisha goli hilo kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika. 

Goli la nyota wa Ufaransa, Ousmane Tembele katika dakika ya 78, lilipeleka vifijo na nderemo Catalunya. 

Fainali za Super cup kwa Mara ya kwanza zimechezwa nje ya Uhispania tangu kuanzishwa Kwake mnamo mwaka 1982. 

Aidha sheria za fainali hizi zimeshuhudia mabadiliko kidogo, kwakua sasa inachezwa mechi moja tu na sio mbili kama ilivyokua awali.Habari Zinazohusiana