Timu ya Yeni Malatyaspor yamuunga mkono Mesut Özil

Timu ya kabumbu ya Yeni Malatya yamuunga mkono Mesut Özil

Timu ya Yeni Malatyaspor yamuunga mkono Mesut Özil

Timu ya kabumbu ya Yeni Malatyaspor  yamuunga mkono  mchezaji nyota wa kimataifa Mesut Özil  baada ya kutangaza kuacha kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani.

Mesut Özil alitangaza kuacha kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kutokana na matamshi ya kibaguzi dhidi yake baada ya Ujerumani kuondolewa mapema katika michuano ya kombe la dunia nchini Urusi.

Timu ya Yeni Malatyaspor ilikutana na timu ya Gazişehir ya Gaziantep katika mechi ya kirafiki ambayo lengo lake ilikuwa kujinuo ili kuwa imara katika michuano inayotarajiwa katika msimu ujao.

Wachezaji wa timu ya Yeni Malatyaspor  waliingia uwanjani wakiwa wamevalia flana zilizokuwa na picha ya Mesut Özil  Jumamosi kabla ya kuanza mechi hiyo.

Katika flana hizo kulikuwa na ujumbe wa kukemea ubaguzi.Habari Zinazohusiana