Mwanfunzi kutoka Tanzania ashinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Capoeira Uturuki

Abdallah Tindwa, mwanfunzi na mwanamichezo kutoka nchini Tanzania amejishindia medali ya dhahabu   katika mashindano ya Capoeira yaliofanyika mjini Ankara  nchini Uturuki

Mwanfunzi kutoka Tanzania ashinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Capoeira Uturuki

Abdallah Tindwa, mwanfunzi kutoka Tanzania ashinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Capoeira Uturuki.

Abdallah Tindwa, mwanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Marmara  mjini Istanbul amejishindia medali ya dhahabu katika mashindano ya mchezo wa Capoeira yalioandaliwa na kufanyika mjini Ankara nchini Uturuki.

Abdallah Tindwa ni mwanafunzi kutoka nchini Tanzania ambae alichagua kuendelea na masomo yake nchini Uturuki akiwa na kipaji katika mchezo wa Capoeira ambapo pia amejikusanyia mashabiki.

Mashindano hayo  ya mzunguko wa mwisho yalijumuisha  vilabu vyote vya mchezo huo nchini Uturuki.

Mashindano hayo yalianyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Hacettepe  hapo Jumapili mjini Ankara.

Capoeira ni mchezo  wa mapigano na sarakasi ambao chimbuko lake ni nchini Brazil.

Mchezo huo ulipata umaarufu mkubwa katika mataifa ya Afrika Mashariki baada ya kuonekana katika filamu kongwe ya “Only the Strong”  ya muigizaji  Mark Dacascos.Habari Zinazohusiana