Levante yazima ndoto za Barcelona

Ndoto za klabu ya Soka ya Barcelona za kumaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote zilizimwa Jana na timu ya Levante

Levante yazima ndoto za Barcelona

Ndoto za klabu ya Soka ya Barcelona za kumaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote zilizimwa Jana na timu ya Levante. 

Mabingwa hao wapya wa Hispania, mpaka Jana walikua wamecheza jumla ya michezo 43 bila kupoteza wowote. Kipigo cha goli 5-4 kutoka kwa Levante kilimaanisha ndoto hizo zimezimwa.

 

Levante waliuanza mchezo huo kwa kasi kubwa na kuwapelekea Barcelona mashambulizi makali ambapo walifanikiwa kuwaongoza kwa Magoli 5 kwa 1 mnamo dakika ya 53. 

 

Vijana wa Catalunya walianza kurudi mchezoni na kufanikiwa kurejesha Magoli matat u zaidi, lakini hayakuwatosha walau kupata sare. 

 

Barca wanasubiri mchezo wao wa mwisho watakaoupiga katika dimba lao la Camp Nou huku wakiwa tayari wameshatawazwa ubingwaHabari Zinazohusiana