Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo 

Ni mwaka mzima umepita na kumekua na mengi katika ulimwengu wa michezo 

Kuna walioshinda na kuna walioshindwa

 

Tukitizama kati ya matukio yaliyoleta majonzi katika ulimwengu wa michezo ni kifo cha mbeba vyuma maarufu Naim Süleymanoğlu.Licha ya kuwa aliweza kubeba uzito mkubwa maishani mwake,siku ilifika na akaiaga dunia.

Jina hili daima litakumbukwa kwani alikuwa na bingwa.Aliweza kujipatia ubingwa mara nane na kuvunja rekodi ya dunia mara arobaini na sita.

 

Tukitizama upande wa riadha,ushindi wa Ramil Guliyev hautosahaulika kwani aliweza kushinda katika mbio za mita 200 na kuipatia medali ya dhahabu kwa mara ya kwanza katika mchezo huo.

Wakati huo huo Yasmani Capello alijipatia medali ya shaba katika mbio za mita 400.

 

Ukisikia jina la Usain Bolt unakumbuka riadha za mita 100.Bolt ambae alikuwa akishinda mara kwa mara kwani ilikuwa hakuna mwanariadha mwenye uwezo wa kumpiku uwanjani.Lakini Usain Bolt hakumaliza safari yake ya uanariadha kwa furaha.

Bolt hakuwahi kujua angeshindwa kupata medali ya dhahabu na badala yake ikachukuliwa na mpinzani wake Justin Gatlin.

Mashabiki wengi hawakuweza kuamini kama Gatlin angeweza kumshinda Bolt Lakini ndivo ilivyokua.

 

Nchini Jamaica ambako ndo ametokea Bolt,sanamu limejengwa kuashiria ushindi wa mwanariadha huyo na kuvunja rekodi ya dunia mara arobaini na sita.Mchezaji huyo mwenye medali 11 za dhahabu amejengewa sanamu lake katika mji mkuu wa Kingstone ili aweze kukumbukwa milele.

 

Tukitizama mchezo wa tenisi majina ambayo yamesikika sana mwaka 2017 ni Federer,Nadal,Murray na Djokovic.Kutokana na kupatwa na majeraha,Murray na Djokovic walimaliza msimu wao mapema.Baada ya mashindano ya Roland Garros,Wawrinka nae alilalamika kupatwa na majeraha.

Federer nae alirudi katika mchezo huo kwa mbwembwe baada ya kutokuwa uwanjani kwa muda wa miezi sita.

 

Katika mashindano ya tenisi nchini Marekani,Rafael Nadal alishinda kwa kumfunga Kevin Anderson.Mechi Nadal aliyocheza na Wawrinka katika mashindano ya Roland Garros ilikuwa muhimu sana.

Nadal alishinda mashindano ya Roland kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 18 na amevunja rekodi kwa kupata ubingwa huo mara    Kumi.

 

Katika mashindano ya Wimbledon,Roger Federer alimshinda mwenzake Marin.Federer alizidi kuonyesha uwezo wake.

Kwenye mashindano ya tenisi Australia,majina mawili makubwa yalikua ni Federer na Nadal ambapo ubingwa mwishoni ulichukuliwa na Federer.

Wachezaji hawa wawili pia walipata fursa ya kucheza kwa pamoja katika mashindano ya kombe la Laver.Katika fainali Federer alicheza na Nadal dhidi ya Sam Querrey na Jack Sock.Timu ya Nadal na Federer kama kawaida iliondoka na ushindi.

Katika msimu wa mchezo huo,Rafael alishindwa mara nne jambo linalomfanya Roger Federer kuwa mchezaji tenisi bora.

 

Turudi katika mchezo wa kuendesha magari,Lewis Hamilton amekuwa bingwa wa dunia.Katika mashindano ya Rally,Sebastian Ogier amejipatia ushindi.Katika mashindano ya Moto GP Marc Marquez amepata ubingwa huku Lucas Mahias akiwa mshindi Supersport.

 

Timu ya mpira wa kikapu ya Fenerbahçe imekuwa bingwa wa ulaya baada ya kushinda 80-86 dhidi ya olimpyakosu.

Timu ya taifa ya Slovenia imepata ubingwa baada ya kuishinda Serbia 93-85.

 

Timu ya mpira wa kikapu ya Vakif Bank imeishinda timu ya Rexona ya Brazil kwa 3-0 na kuwa mabingwa.

 

Timu ya Volleyball ya wanawake ya Bursa imeshinda katika mashindano ya Ulaya.Timu ya Doğu Üniversitesi imeshinda Euro Cup.

 

Huku Messi akiwa amepewa adhabu ya kutocheza mechi nne,mwenzake Ronaldo alichaguliwa kama mchezaji bora wa mwaka.

 

Chris Froome ameshinda katika mashindano ya kuendesha baiskeli ya Ufaransa pamoja na Uhispania.

Tunasubiria mwaka ujao wenye msisimko mpya,na rekodi mpya zitavunjwa.

 

Kwa sasa tunawatakieni nyote mwaka mpya wenye furaha na mafanikio 

Kheri ya Mwaka Mpya

 

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.Habari Zinazohusiana