Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Leo katika ulimwengu wa michezo 

Mchezo wa mashindano ya pikipiki umefikia mwisho.Mchezo wa Formula 1 unafikia ukingoni sasa.Mashindano ya Ulaya Superstock 1000 nayo yamefikia mwisho.

 

Mashindano ya 16 ya Moto GP yalifanyika Australia.

 

Katika mashindano ya Formula 1 ya 17,Lewis Hamilton amejinyakulia ubingwa kwa mara nyingine tena na kuliongezea jina lake sifa madhubuti.

 

Mashindano hayo yalifayika Texas nchini Marekani ndani ya uwanja wa Austin kwa umbali wa mita 5513 kwa raundi 56.Mchezaji mahiri Lewis Hamilton alimaliza mashindano hayo akiwa wa kwanza na kuwa bingwa mara nne mfululizo.

 

Mpinzani wa Hamilton ,Sebastian Vettel yeye alimaliza mashindano hayo akiwa katika nafasi ya pili.Kutokana na adhabu ya sekunde tano aliyopewa Max Verstappen ya kutoka nje ya uwanja,Raikkoken aliweza kujinyakulia nafasi ya tatu.

 

Mashindano ya Formula 1 yatafanyika nchini Mexico.Endapo Hamilton Vetteli ataweza kushinda katika raundi ya 18 basi itakuwa ni mara yake ya nne kuwa bingwa katika mashindano hayo.

 

Matokeo yalikuwa ni Lewis Hamilton katika nafasi ya kwanza,Sebastian Vettel wa pili,Valtteri Bottas nafasi ya tatu,Daniel Ricciardo wa nne na Kimi Raikkoken katika nafasi ya tano.

 

Mashindano hayo yatafanyika Grand Prix Mexico katika wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba.

 

Katika mashindano ya Moto GP ya Australia Marc Marquez ndie amejinyakulia ushindi.

Marc Marquez aliyeshindwa katika mashindano hayohayo ya mita 400 ndani ya raundi 27 katika kisiwa ch Philip ameweza kujipatia ushindi katika raundi ya 21 na kumaliza msimu huo kama bingwa.Hii ni mara ya sita kwa mchezaji huyo kupata ushindi katika msimu huu na mara 35 kwa yeye kuwa wa kwanza katika maisha yake kama mchezaji ws Moto GP.

 

Katika mashindano ya 16,Valentino Rossi amekuwa wa pili kwa sekunde 1.7,Maverick Vinales wa tatu kwa sekunde 1.8.

 

Matokeo yalikuwa kama hivi

Marc Marquez pointi 269

Andrea Dovizioso 236

Maverick Vinales 219

Valentino Rossi 188 na katika nafasi ya tano 

Daniel Pedrosa 174.

 

Marc Marquez anakarinia kupata ushindi katika mashindano ya nne ya kutafuta ubingwa baada ya kuwa wa katika raundi ya 16.Ni mashindano mawili tu yamebaki.

Mashindano ya 17 yatafanyika Grand Prix Malayım 29 Oktoba.

 

Tutatizame mashindano ya Ulaya ya Superstock 1000.Mashindano hayo yalifanyika katika uwanja wa Jerez nchini Uhispania.Katika raundi ya 15,Ruben Rinaldi aliweza kuwa wa kwanza kwa pointi 138.

Katika msimu wa pili wa mchezo huo Toprak Razgatlıoğlu amekuwa wa pili kwa pointi 130,Florian Marino wa tatu kwa pointi 120.

 

Mashindano kabambe kabisa ya kuendesha baiskeli ya Ufaransa 2018 yamezinduliwa rasmi mjini Paris.

Katika pwani ya Atlantiki mashindano hayo yataanza Vendee Ufaransa kwa raundi 21 kwanzia 7-29 Julai.Wachezaji watanyonga baiskeli katika milima tofauti hadi kufikia kilele.

Mashindano hayo yataishia Champs Elysee mjini Paris.

 

Na kwa kumalizia, mchezaji maarufu wa Golf Tiger Woods anajiandaa kurudi ulingoni baada ya kuwa mbali na mchezo huo kutokana na sababu za kiafya.Meneja wake ametangaza kurudi kwa Tiger Woods na kusema ataanza kushiriki katika mashindano kidogo kidogo.

Tiger Woods aliyefanyiwa upasuaji mara nne ndani ya miaka mitatu ni mchezaji aliyewahi kupata ubingwa mara 14 na ni mchezaji anaejulikana kwa kupata ushindi mara kibao.

 

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.Habari Zinazohusiana