Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Leo katika ulimwengu wa michezo 

Wafuatiliaji wa mchezo wa tenisi siku zote hutizama pande mbili.Upande wa Nadal na ule wa Federer.Siku zote mechi kati ya wachezaji tenisi hawa mashuhuri hutizamwa na mashabiki wengi.Federer na Nadal wamekuwa wakishinda katika mechi tofauti.Nadal aliweza kuwa mshindi katika mfululizo wa mechi kumi na sita,Federer nae aliweza kushinda katika mashindano ya Grand Slam.Je Nadal ataweza kujinyakulia ushindi katika mashindano ya tenisi Miami,Australia,Indian Wells dhidi ya Shangay au atakubali kwa mara ya nne Federer aweze kupata ushindi?

Wachezaji hawa wawili wanapata shida kidogo hasa katika mechi za nusu fainali.

Nadal aliweza kumshinda Marin Cilic kwa kupata matokeo 2-0 kwa seti 7-5/7-6.Federer nae aliweza kushinda katika mashindano Marekani kwa matokeo 2-1 ndani ya seti 3-6/6-3/6-3.

Na sasa fainali imewadia.Nadal,mshindi wa mechi kumi na sita mfululizo dhidi ya Federer ambae ameshinda mara tatu kuliko Nadal.Je mwisho wa mechi utaleta matunda gani?.Hii ni mechi ambayo ni vigumu sana kutabiri mshindi kama ilivyo katika mechi nyingine.

Kuna wanaomshabikia Federer na vilevile wale wanaomshabikia Nadal.

Federer alianza kwa kushinda katika seti ya kwanza 6-4.Seti ya pili ilionekana rahisi pia kwa Federer na akapata pointi 6-3 hali iliyompelekea kupata matokeo ya 2-0 na kushinda mechi ya Shangai kwa mara ya pili.

Hii ni mara ya 94 kwa mchezaji Federer kupata ubingwa hali inayomfanya alingane na mchezaji maarufu Ivan Lendi.Wachezaji hawa wawili wanakuja baada ya mchezaji tenisi namba moja aliyepata ubingwa mara 109 Jimmy Connors.

 

Sharapova aliyepewa adhabu ya kutocheza kwa muda wa miezi 15 baada ya kukutwa anatumia madawa ya kuongeza nguvu amerudi uwanjani na kushinda katika mashindano ya Tianjin nchini China.Katika mechi ya mwisho aliweza kumshinda Aryna Sabalenka kwa seti 7-5/7-6 na kupata matokeo 2-0.Mchezaji huyo amekuwa bingwa wa WTA baada ya kupigwa marufuku kucheza kwa muda wa miezi 15.

Sharapova amewaonyesha mashabiki kuwa yeye bado ni bingwa.

Uturuki imetayarisha mashindano ya kuendesha baiskeli kabambe.Mashindano hayo yalianzia Alanya na kuendelea mpaka Istanbul.Diego Ulissi ndio amekuwa mshindi.

Katika raundi ya sita ya mashindano hayo Istanbul-Istanbul Sam Bennet alichuana na Edward Theuns.Wakati wa mashindano Sam Bennet alianguka na kumpelekea Edward Theuns kushinda katika raundi hiyo.Lakini mwisho wa yote ubingwa huo umechukuliwa na Diego Ulussi.Jesper Hansen amechukua nafasi ya pili,Fausto Masnada nafasi ya tatu.

 

Na sasa tutizame mashindano ya pikipiki.Ubingwa wa mashindano ya 15 ya Moto GP umechukuliwa na Andrea Dovizioso.Mashindano hayo yalifanyika Grand Prix Motegi Japan ndani ya kilomita 4.8 na raundi ya 24 ikafanyika Twin Ring Motegi nchini Japan.

Baada ya Marc Marquez,Davizioso amekuwa wa kwanza katika mashindano ya Moto GP kwa mara ya tano.

Matokeo ni kama hivi:

Marc Marquez 244

Andrea Dovizioso 233

Maverick Vinales 203

Dani Pedroso 170

Valentino Rossi 168 pointi.

Mashindano ya 16 yanatarajia kufanyika Grand Prix 22 Oktoba.

 

Tutizame mpira wa kikapu.Mchezaji mashuhuri Michael Jordan ameikashifu Super team na kusema inaiharibia NBA.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 54 ambae pia ni mmiliki wa Charlotte Hornets amesema kuwa      franchises nyingine 28 zinaweza kuwa jalala.

 

Tutizame matokeo ya Ligi ya Ulaya

Cristal Palace -Chelsea 2-1

Watford-Arsenal 2-1

Liverpool-Manchester 0-0

 

Tukitizama Italia

Juventus-Lazio 1-2

 

Ujerumani 

Dortmund-Leıpzıg 2-3

 

Uhispania 

Atletico Madrid-Barcelona 0-0

 

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.Habari Zinazohusiana