Bale, Sanchez, Mehrez na Dzeko kutocheza kombe la dunia Urusi 2018

Baadhi ya nyota wa mpira wa miguu kutoka Asia, Afrika, Ulaya, Amerika hawatashiriki kombe la dunia la FIFA litakalofanyika Urusi 2018.

Nchi zitakazocheza kombe la dunia zinaanza kujulikana kufuatia matokeo ya kuwania nafasi za kwenda Urusi.

Miongoni mwa nyota watakaokosa kucheza kombe la dunia ni Gareth Bale anaechezea Real Madrid baada ya timu yake ya taifa ya Walles kushindwa kupata tiketi ya kushiriki kombe la dunia.

Mbali na mlinda lango kutoka Slovenia, Jan Oblak, mholanzi Arjen Robben, wachezaji wawili wa Chili Arturo Vidal na Alexis Sanchez, David Alaba wa Austria, Edin Dzeko na Miralem Pjanic kutoka Serbia hawatashiriki kombe la dunia huko Urusi baada ya nchi zao kushindwa kupatia tiketi.

Vile vile Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Henrik Mkhitaryan kutoka Armenia , Riyad Mehrez na Islam Slimani kutoka Algeria pia hawataonekani viwanja vya kombe la dunia.Habari Zinazohusiana