Simeone na Klopp wagombea ukufunzi huko Bayern Munich

Simeone anaweza kusajiliwa na klabu ya  Ujerumani ya Bayern Munich kuwa mkufunzi wake baada ya kocha wake wa zamani Anceloti kutimuliwa.

Simeone na Klopp wagombea ukufunzi huko Bayern Munich

 

Habari kutoka gazeti la Kiingereza "The Sun", zinasema kuwa  raia wa Argentina, Diego Simeone, ambaye ni kocha wa klabu ya huko Uhispania ya Atletico Madrid anaweza kusajiliwa na klabu ya  Ujerumani ya Bayern Munich kuwa mkufunzi wake baada ya kocha wake wa zamani Ancelotti kutimuliwa.

Kwa upande wake,gazeti la Uhispania la «As», limethibitisha habari hiyo, na kusema kuwa mazungumzo yameanza baina ya Bayern Munich na Diego Simeone kuhusu usajili wake.

Nayo magazeti ya Ureno yanasema kuwa Diego Simeone na Byern Munich wakishindwa kukubaliana, basi timu hiyo inapanga kumfuata mkufunzo mjeremani,Jurgen Klopp, ambaye ni kocha wa timu ya Liverpool.

Ikumbukwa kuwa Bayern Munich ilimtimua kocha wake mtaliano,Carlo Ancelotti, baada ya kujikuta kitanzini kwa kuchapwa magoli 3 kwa nunge na timu ya PSG kutoka ufaransa kwenye uwanja wa Pelouse du Parc des Princes mjini Paris, kwenye michuano ya ligi ya washindi barani Ulaya ama Europe champions league.

 Habari Zinazohusiana