Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

 

Wapenda mchezo wa tenis wamekuwa wakitizama mashindano kati ya Federer na Nadal kwa muda mrefu.Kwa wapenda tenisi haijalishi ni nani hushinda katika mechi kati ya mabingwa hao wawili kwani wote hushabikiwa na hupendwa sana.

Mara hii imekuwa ni tofauti kwani Federer na Nadal hawakushindana kama wapinzani bali wamecheza katika timu moja kwenye mashindano ya Laver Cup.Kama kawaida Federer alifanikiwa kumshinda Sam Qeerreyi huku Nadal akiwa amemshinda mpinzani wake Jack Sock.

Katika seti ya kwanza Federer na Nadal walishinda kwa alama 6-4.Katika seti ya pili timu ya Querrey na sock ilipata pointi 6-1.Mashabiki wa Federer na Nadal walipatwa ma shauku kubwa hasa baada ya mchezo wa seti ya pili kuisha kwani kulikuwa na uwezekano wa Federer na Nadal kushindwa.

Hata hivyo Federer na Nadal hawakuvunja matumaini ya mashabiki zao na wakafanikiwa kushinda mechi kwa alama 10-5.

Katika mashindano ya tenisi kati ya timu za Ulaya dhidi ya nchi nyinhine Nadal aliweza kumshinda mchezaji John Isner na kupata pointi 12-9.Katika mechi ya mwisho kati ya Frderer na Kyrgios ,Federer alimaliza mechi kwa pointi 4-6/7-6 na 11-9.Hii ilimsaidia yeye kujipatia ushindi kwa pointi 15-9.

Katika mashindano ya tenisi ya Laver Cup yaliyoandaliwa Prag ,Federer na Nadal walijipatia ushindi kwa kupata pointi 15-9.Makapteni wa mchezo huo walikuwa ni Bjorn Borg na John McEnroe.

Tutizame mashindano ya tenisi ya wanawake.Katika mashindano ya Pacific Muguzura aliweza kumshinda Wozniack.Kwenye mashindano yaliyoandaliwa Tokyo Wozniack aliweza kumshinda Muguzura kwa 6-2 na 6-0 Katika seti mbili.Matokeo ya mwisho yalikua ni 2-0.

Katika mashindano ya kuendesha pikipiki ya MotoGP Marc Marquez ndie amejinyakulia ushindi.Mashindano hayo yalifanyika Uhispania ndani ya kilomita 5.1 kwa raundi 23.Katika mashindano ya 14 Dan Pedrosa aliweza kuwa wa pili,Jorge Lorenzo wa tatu.

Marc Marquez alimaliza kwa pointi 224,Andrea Dovizioso 208,Maverick Vinales 196,Dani Pedrosa 170 na Valentino Rossi 168.

Mashindano ya 15 yanatarajia kufanyika Grand Prixi Japan 15 Oktoba.

Katika mashindano ya supersport Kenan Sofoğlu ameweza kujiongezea sifa kwa kupata pointi 145.

Tutizame mashindano ya mpira wa wavu wa wanawake kati ya Azerbaijan na Georgia.Mashindano hayo yameshirikisha timu Za taifa za Urusi,Ukraine na Bulgaria ndani ya kundi C.

Na katika mpira wa kikapu timu ya Fenerbahçe Doğuş imeishinda CSKA Moscova kwa 76-72 na kuwa mabingwa wa Zadar Cup.

Katika mashindano ya mbio ya Belin Eliud Kipchoge kutoka Kenya amejipatia ushindi kwa mara ya pili.

Mwendesha baiskeli kutoka Slovakia Peter Sagan amejipatia ushindi katika mashindano ya kumtafuta bingwa wa mchezo huo.Sagan amevunja rekodi kwa kushinda mara tatu mfululizo katika mashindano yaliyoandaliwa Mjini Bergen nchini Norway.

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.

 Habari Zinazohusiana