Juventus de Turin walazimika kwenda sare ya 2-2 na Atalanta Bergane

Juventus wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya SSC Napoli, wanaoshikilia uskani baada ya kuwalaza Cagliari kwa 3-0. Huku Atalanta wakiwa nafasi ya 11 na pointi 9.

Juventus de Turin walazimika kwenda sare ya 2-2 na Atalanta Bergane

 

Atalanta Bergane na Juventus de Turin wameenda sare ya kufungana 2-2, siku ya saba ya michuano ya ligi kuu ya Italia daraja la kwanza.

Juventus de Turin ama Bibi kizee, kwa jina la utani wamelazimika kwenda sare kwenye uwanja wa Atalanta.

Vijana wa kocha Allergi, matumaini yao yakutofungwa yamezimwa wakiwa Bergame.

Hata hivo wachezaji wa Bianconeri yaani weusi kwa weupe, kwa jina lingine la Juventus, kuanzia dakika ya 24 ya mchezo wameweza kuwalaza Atalama kwa magoli mawili kwa nunge, kupitia mchezaji Bernardeschi mnamo dakika ya 21 , na Higuain mnamo dakika ya 24.

Atalanta Bergane iliweza kurudisha magoli yote hayo mawili kupitia mchezaji Caldara, baada ya mlinda lango Buffon kushindwa kudhibiti mpira kwenye dakika ya 31, na dakika ya 67 Cristante akiangiza goli la kichwa la kusawazisha.

Kutokana na matokeo hayo,  Juventus wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya SSC Napoli, wanaoshikilia uskani baada ya kuwalaza Cagliari kwa 3-0. Huku Atalanta wakiwa nafasi ya 11 na pointi 9.

 Habari Zinazohusiana