Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo
Miongoni mwa tutakayoyaangazia leo hii ni pamoja na hatua za makundi za michuano ya kuwania kushiriki kombe la dunia mwaka 2018,  michuano ya ubingwa wa mpira wa kikapu barani Ulaya, bila kusahau mashindano ya mbio za magari maarufu kama formula one, na mwisho kabisa tutagusia mashindano ya wazi ya mchezo wa Tenis Marekani.

Wiki hii, Nchi zote barani Ulaya ziliingia viwanjani kuwania nafasi ya kufuzu kwenda fainali ya kombe la dunia ya mwaka 2018 ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Urusi. Nchi za Ulaya zimewekwa katika makundi 9 tofauti.
Ufaransa inaongoza kundi A ikiwa na alama nyingi zaidi huku ikifuatiwa na timu ya taifa ya Uswisi. Uholanzi inainyemelea kwa mbali nafasi ya pili ya kundi hilo. Ufaransa iliiadhibu timu ya uholanzi kwa goli 4 kwa 1 huku ikienda sare na timu ya Luxernborg. 

Timu ya Taifa ya Uswidi ndio inayoongoza kundi B huku ikifuatiwa kwa karibu Sana na timu ya Ureno. Timu hizi zinashindania nafasi ya kwanza ya kundi hilo. 

Ujerumani yenyewe inaongoza kundi C huku ikiwa imeipita timu ya Ireland Kaskazini kwa alama 5 katika nafasi ya pili.
Ushindani mkubwa katika kundi D unazifanya timu tatu ziwanie nafasi mbili za mwanzo. Serbia inaongoza ikifuatiwa na Ireland huku Wales ikiwa nafasi ya tatu.
Kundi E linawakutanisha miamba wa Poland, Montenegro na Denmark ambazo zinawania nafasi ya pili.
Kundi F linaongozwa na Uingereza ikifuatiwa na Slovakia, huku timu za Uhispania na Italia zikishindania nafasi ya kwanza ya kundi G.
Ubelgiji ndo inakua nchi ya kwanza kujihakikishia nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kushinda Michezo saba na kutoa suluhu moja hivyo wakajikusanyia jumla ya alama 22. Bosnia Herzegonia inashika nafasi ya pili ya kundi hilo H ikiwa na alama 14 Huku Ugiriki ikiwa karibu kabisa kwa Alama 13. 
Kundi I linakutana na ushindani mkubwa mno wakati Ukraine na Croatia zikiwania nafasi ya kwanza, Uturuki na Island zinatoana jasho kwa nafasi ya pili. 
Mechi hizi za mtoano zinatarajiwa kuisha mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.

Naam na sasa tuyatupie macho mashindano mengine yenye ushindani mkubwa barani Ulaya. Ni mashindano ya ubingwa wa mchezo wa mpira wa kikapu barani humo. Kutakua na makundi manne ambapo kila kundi litakua na timu 6. Timu zitakazoshika nafasi nne za mwanzo katika kila kundi zitaingia katika hatua inayofuata ya mtoano. Fainali za mashindano haya zitafanyika jijini Istanbul.

Kundi A litazikutanisha timu za Slovenia, Poland, Island, Ugiriki, Ufaransa na Finland, wakati timu za Ujerumani, Ukraina, Litvan, Georgia, Italia na Israel Watatoana jasho katika kundi B. Kundi C lenyewe linaundwa na timu za Hungary, Croatia, Montenegro , Romania na Jamhuri ya Czech. Kundi D ni la Uturuki, Ubelgiji, Uingereza, Urusi, Serbia na Latvia.

Bado tunaendelea kuliangalia bara la Ulaya, hatuna budi kuingia katika mashindano ya kuendesha magari . Mwingereza Lewis Hamilton ameibuka mshindi wa hatua ya 13 ya mashindano ya magari. Mashindano haya yalifanyika nchini Italia na yalikua na jumla ya kilomita elfu 5 mia 7 na 93. Hamilton sasa anashika nafasi ya sita katika mashindano haya ya 201 huku ikiwa ni mara ya 59 anakua wa kwanza katika maisha yake ya mashindano. 

Valtteri Bottas raia ya Finland alishika nafasi ya pili ya duru hii ya 13, huku Mjerumani Sebestien Vettel akishika nafasi ya tatu.
Sasa Lewis Hamilton amefikisha jumla ya alama 238 na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa hatua zote za mashindano hayo..
1. lewis Hamilton 238 
2. Sebastian Vettel 235
3. Valtteri Botas 197
4. Daniel Ricciardo 144
5. Kimi Raikkonen 138
Duru ya 14 ya formula one inatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 17 Septemba huko nchini Singapore. 
Habari nyingine inayohusiana na mashindano ya magari ni ile ya Valentino Rossiden. Rossi ambaye wengi walidhani atakua bingwa wa mashindano ya GP amepata majeraha baada ya kuvunjika mifupa kadhaa kufuatia ajali wakati akifanya mazoezi. Baada ya kukamilika matibabu yake, madaktari katika hospitali ya Ancona walieleza kuwa Rossi atahitaji kupumzika kwa siku 30 hadi 40 ili apone vizuri. Rossi ambaye anashika nafasi ya nne katika mashindano hayo ya GP ambayo yamebakiza hatua 6 kumalizika, atashindwa kushiriki mashindano ya tarehe 10 Septemba. Mshindi huyo wa mashindano ya 9 ya Moto GP pia aliwahi kuvunjika mguu katika mashindano ya mwaka 2010.

Tukigeukia upande mashindano ya tenis yanayoendelea huko nchini Marekani, mastaa wakubwa wengi wameshindwa kushiriki kutokana na majeruhi. Murray, Djokovic, Wawrinka, Nishikori, Raoniç ni miongoni mwa majina makubwa yalokosekana. Kutokuepo kwa majina haya katika mashindano ya wazi Marekani, kunawapa fursa wachezaji wachanga kuibuka katika mchezo huo. Kwa upande mwingine, mashindano haya hameshangaza wengi kwakua imewaondoa nyota waliongaa katika mashindano ya Wimbledon. Wakali kama Ferrer, Vinolas, Tsonga, Zverev, Isner na Haase wameondolewa katika hatua za awali kabisa. Nadal na Federer wanatarajiwa kukutana katika mchezo mkali wa nusu fainali. 

Kwa upande wa nyota wa kike wa tennis pia, wametolewa mapema katika mashindano hayo. Simona Halep anayeshikilia nafasi ya pili duniani ametolewa katika duru ya kwanza ya mchezo. Wengine kama Radwanska, Kerber, Wozniacki na Kuznetsova wameaga mashindano hayo mapema. Sharapova ambaye alishiriki mashindano hayo kwa mwaliko maalum, ametolewa katika hatua ya tatu.
Mashabiki wengi wanangojea kwa hamu mechi za fainali zitakazochezwa mwisho wa wiki hii.
Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.


Habari Zinazohusiana