Wapalestina wawili wafariki katika handaki linalounganisha Gaza na Misri

Wapalestina wawili wafariki  katika handaki linalounganisha Ukanda wa Gaza na Misri

handek.jpg

 

Wizara ya mambo  ya ndani ya mamlaka ya wapalestina imefahamisha  mapema Jumatatu kuwa  wapalestina wawili akiwemo afisa mmoja wa jeshi la Polisi wamefariki katika handaki linalounganisha Ukanda wa Gaza na Misri.

 Katika taarifa iliotolewa na uongozi wa Ukanda wa Gaza uliopo chini ya chama cha Hamas,  afisa mmoja wa jeshi la Polisi  ambae alikuwa akfahamika kwa jina lla Abedlhamid Akr ndie aliefariki katika katika handaki hilo .

Wapalestina hutumia mahandaki kwa  ajili ya  uchukuzi  kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Taarifa zimefahaamisha kwamba tukio hilo limetokea katika operesheni ya kulinda usalama Jumapili usiku.

Kikosi cha kutoa huduma ya kwanza  kimefahamisha kuwaokoa askari wengine wawili waliokuwa wamekwama katika handaki hilo.

Taarifa nyingine zimefhamisha kuwa wapalestina 9 hawajulikani walipo tangu Jumamosi baada ya  jeshi la Israel kulipua handaki wakati ambapo walikuwa wakisafirisha  bidhaa katika  handaki hilo. Hakuna taarifa yeyote ambayo imetolewa na jeshi la Israel kuhusu tukio hilo.Habari Zinazohusiana