Uturuki yaitolea wito Uchina kuheshimu haki za binadamu

Kuhusiana na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na mamlaka nchini China dhidi ya waturuki na waislamu wa Uyghur, Uturuki imeitaka China kuheshimu haki za binadamu.

Uturuki yaitolea wito Uchina kuheshimu haki za binadamu

Uturuki imeitolea wito Jamhuri ya watu wa china kutokana na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na nchi hio dhidi ya raia eneo la Uyghur.

Wito huo umetolewa katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Uturuki Hami Aksoy.

Katika taarifa hiyo Aksoy alisema sheria zinazovunja haki za msingi za binadamu zinazotekelezwa dhidi ya waturuki na waislamu wengine wa eneo linalojitawala la Uyghur , Sinjan hasa katika miaka hii miwili ya mwisho zinapaswa kutazamwa na jamii ya kimataifa.

Taarifa hio inaendela kusema kwamba sio siri tena kwamba watu zaidi ya milioni moja wanashikiliwa, na kwamba yamekuwepo makambi na magereza ya kuwakusanya waturuki ili kuwatesa na kuwabadilisha idiolojia za kisiasa.

Taarifa hio imeendelea kusema kwamba ni aibu kubwa kwa serikali ya China kutumia aina ya siasa inayotumia dhidi ya watu wa Uyghur ambao wengine wana asili ya Uturuki.

Taarifa hio imesema kwamba Uturuki inazitaka mamlaka nchini China kukomesha mara moja vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu dhidi  watu wa Sinjan. Na pia Uturuki inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na Umoja wa mataifa kutafuta utatuzi wa janga linalowakabili watu wa eneo la Sinjan.

 


Tagi: Uyghur , China , Uturuki

Habari Zinazohusiana