Maandamano ya kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Uyghur Marekani

Maandamano dhidi ya China yafanyika nchini Marekani kukemea ukiukwaji wa haki za Uyghur

abd cin protesto1.jpg

Maandamano dhidi ya China yafanyika nchini Marekani kukemea ukiukwaji wa haki za  binadamu dhidi ya Uyghur.

 Mkurugenzi wa  kimataifa wa muungano wa jamii ya Uyghur Isa Dolkun asema kuwa kwa muda wa miaka mingi  jamii ya Uyghur imekuwa ikinyanyaswa.

Maandamano makubwa dhidi ya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Uyghur nchini Chşna yafanyika  mjini New York nchini Marekani.

Waandamanaji  wakiwa na bendera  za Uturuki na Turkstan Mashariki  pamoja na waturuki  wa Uyghrur wanaoishia nchini Marekani wameandamano mbele ya ubalozi mdogo wa Chini mjini New York kukemea   dhulma wanayotendewa waislamu jamii ya Uyghur Xinjiang.

Waandamanaji walikuwa na mabango ambayo yalikuwa na jumbe za kukemea  dhulma wanayotenedewa  Uyghur.

 Mkurugenzi wa shirika la  waturuki İslam Toplumu Milli Görüş (IGMG) nchini Marekani Ayhan Özmekik amewaambia  waandishi wa habari kuwa lengo la maandamano hayo ni kukemea manyanyaso dhidi ya jamii ya Uyghur.

  Mkurugenzi huyo amekumbusha kuwa  maandamano hayo ni kuonesha ulimwengu unaofumbia macho madhili yanayowasibu Uyghur.

 Kwa kumalizia Isa Dolkun ametolea wito Uturuki , Umoja wa Mataifa na Marekani  kulitazama suala la Uyghur waliofungwa na kunyanyaswa bila ya hatia yeyote ile.

 Habari Zinazohusiana