Uturuki yakemea China kwa ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Uyghur

Uturuki yakemea vikali  ukiukwaji wa haki za binadamu unaotendewa jamii ya Uyghur na China

Uturuki yakemea China kwa ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Uyghur

Uturuki yakemea vikali  ukiukwaji wa haki za binadamu unaotendewa jamii ya Uyghur  nchini China.

Uturuki imetolea wito  China h kuheshimu  haki za binadamu  na kuheshimu haki za waturuki wa jamii ya Uyghur.

Katika wito huo Uturuki imeitaka pia China kufunga kambi zilizofunguliwa kwa ajili ya kuwafunga wachina wa jamii ya Uyghur.

Msemaji wa wizara ya  mambo ya nje Hami Aksoy amesema kuwa  suala hiöo la ukukwaji wa haki za binadamu  lichukuliwa na umuhimu mkubwa.

Matendo ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhid ya waturuki wa jamii ya Uyghur na waislamu  katika eneo la Xinjiang vimeongezeka  katika kipindi cha maiaka miwili ya iliopita.

Hami Aksoy amesema kuwa watu zaidi ya milioni moja wa jamii ya Uyghur  wanazuiliwa  kimakosa  na kuteswa katika maeneo walipofungwa.

Watoto na wanawake waliotengenishwa na familia zao  wamekuwa yatima  kutokana na kwamba hawajui waliko wazazi wao.Kuona kambi za halaiki katika karne ya 21, kambi ambazo waturuki jamii ya Uyghur wanateswa ni aibu kubwa kwa ulimwenguni wa kisasa.

Tamko hilo kutoka katika ofisi za wizara ya mambo ya nje  limefahamisha kuwa  China imekwisha  fahamishwa kuhusu msimamo wa Uturuki kuhusu madhila yanayowasibu waislamu wa jamii ya Uyghur Xinjiang.

Aksoy ameskitishwa na taarifa  ya kifo cha mtunzi wa  mashahiri Abdurrehim Heyit  ambae alikuwa amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka minane ambae amefariki  akiwa gerezani.Habari Zinazohusiana