Moro kuelekea siku za mwangaza

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

Moro kuelekea siku za mwangaza

 

Inawezekana Moro ndio eneo lililodumu katika machungu ya migogoro kwa muda mrefu zaidi katika historia ya binadamu. Machungu hayo yalianza miaka ya 1500. Umwagaji damu, dhulma, ukandamizwaji ni katika machungu walioishi watu wa Moro. Leo hii tumaini jipya limeanza kuonekana. Watoto wa Moro hawatalia tena , siku za kiza wataziacha nyuma, badala ya kuishi yatima wataishi kwa amani.

                                      

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na mada hii...

 

Moro kama ilivyo Palestina, Eritrea, Kashmir na maeneo mengine kunapoonekana dhulma za waziwazi,  ni katika maeneo yanayokumbukwa sana katika dua za kila siku za waturuki. Watu wengi wataikumbuka Moro hasa kutoka katika shairi maarufu lenye kugusa nyoyo la Salih Mirzabeyoğlu “Mwangaza kwa Wapiganaji- Moro uwanja wa mapambano”.

Lakini hivi sasa mustakabali mpya unawakabili waislamu. Katika makala hii tutajaribu kuelezea kura ya maoni iliyofanyika Januari 21.

 

Historia fupi ya Moro  

Kufika na kuenea kwa Uislamu katika visiwa vya Ufilipino hakutofautiani sana na ilivyokuwa katika maeneo mengine ya mashariki ya mbali. Wamoro pia waliufahamu uislamu kupitia kwa wafanyabiashara wa kiislamu waliofika katika maeneo yao.

Waislamu walikuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe mpaka miaka ya 1500.

Moro, vita ya kwanza  baina ya waislamu na wahispania ilianza mnamo mwaka 1521. Baada ya kuanguka kwa Andalusia vita hivi vikawa dhidi ya Ufilipino. Toka kipindi hicho mpaka hivi sasa  vita hivyo  vimekuwa vikiendelea kwa mtindo tofauti. Inaweza kusemwa kwamba vita hivyo vimedumu kwa miaka 500.

Mnamo miaka ya 1900 walio wengi kama sio wote kusini mwa Ufilipino walikuwa ni waislamu. Kutokana na juhudi za makusudi zilizofanywa idadi ya waislamu ikapunguwa sana,kupelekea waislamu kuwa kundi la watu wachache katika maeneo hayo.

Eneo hilo mwanzoni lilitawaliwa na wahispania, nusu ya kwanza ya karne ya 20 Moro ilitawaliwa na wamerakani na kisha baadae ilitawaliwa na wafilipino. Watawala wote hawa waliwaandama waislamu kwa kuwaua au kuwalazimisha wahame eneo hilo.

Mwaka 2016 nilipozuru niliona watu wasio na makazi, ambao walikatazwa kutumia ardhi kitu kilichowapelekea kujenga makazi ya muda juu ya mito ya maji. Waislamu wa Moro katika kujihami na sera zilizokuwa na lengo wa kuwatokomeza mnamo miaka ya 1960 walianzisha vuguvugu la mabadiliko. Harakati hizo kwa vipindi tofauti zimekuwa zikiendeshwa na taasisi tofauti. Kiongozi wa harakati za ukombozi wa waislamu Selamet Hashim alianzisha mazungumzo na serikali ya Ufilipino. Baada ya kifo cha Hashim mnamo mwaka 2003, Haj Murat Ibrahim alichukua nafasi ya uongozi na kuendeleza harakati hizo.

Baada ya miaka 40 ya vita vya ndani vilivyopelekea vifo vya watu laki 1 na elfu 20 pamoja na zaidi ya watu milioni 2 kuyahama makazi yao, Ili kupatia ufumbuzi tatizo hilo serikali ya Ufilipino na Chama cha ukombozi wa waislamu cha Moro (MILF) mnamo mwaka 2012 walisaini  makubaliano. Mnamo mwaka 2014 katika kutunza amani ilianzishwa kamati maalum iliyoitwa “ kamati huru ya Uangalizi”.Mwaka 2014 katika kampeni za uchaguzi wa urais, rais aliyepo madarakani hivi sasa nchini Ufilipino Rodrigo Duterte akiwa mgombea aliahidi kuipa mamlaka kamili Moro.

Matokeo ya kura za maoni na umuhimu wake

Januari 21 mwaka  2019 ilifanyika kura ya maoni ambapo mamlaka kamili ya waislamu wa Moro ilipitishwa kwa asilimia 80. Kutoka hapo itaundwa  serikali ya muda itayoongoza mpaka mwaka 2022.  Serikali hii ya muda itakuwa na wajumbe 80 na itafanya kazi kama aina fulani ya bunge. Serikali hiyo itatambulika kama “Mamlaka ya muda ya Bangsamoro”.

Kwa kupita kwa kura hiyo ya maoni , asilimia 75 ya mapato ya eneo hilo yatabaki katika eneo hilo huku asilimia 25 ikienda kwa serikali kuu.

Waislamu wa Bangsamoro tofauti na Ufilipino wanaweza kutumia sheria za kiislamu. Miongoni mwao wanaweza kuhukumiana kwa sheria za dini ya kiislamu. Wakristo wanaopatikana katika eneo hilo la Moro wanaweza kutumia sheria za Ufilipino kwenye masuala yao. Mambo ya ndani ya waislamu wa Moro yamepatiwa uhuru wa asilimia 100 kutekelezwa na serikali hiyo ya Moro, huku mambo ya nje pamoja na masuala ya usalama yataendelea kubaki chini ya serikali ya Ufilipino.

 

Mahitaji ya waislamu wa Moro

Uungaji mkono wa mchakato wa amani: Kudumisha amani ni suala gumu sehemu yeyote ile duniani. Makundi yanayohasimiana mara zote yapo kwenye hatari ya kuingia tena kwenye mgogogro muda wowote. Kwa ajili hiyo basi ni muhimu sana kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mchakato huo.Kutoka na kwamba rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte anatokea eneo la karibu na Bangsamoro, sehemu kubwa ya utoto wake amekuwa na mahusiano mazuri na watu wa Moro, hilo nalo pia ni fursa kwa mchakato wa amani. Kuhusiana na hilo ili mchakato huu wa amani uendelee inahitajika uungwe mkono na rais Duterte. Inabidi pia umakini uwepo ili mchakato huu usivunjwe na mikono ya Daesh.

Dharura ya misaada ya kibinadamu: Nchi ambayo imekuwa ikipigania uhuru kwa miaka 500. Katika kufikia uhuru huo kuna gharama kubwa ambayo jamii hii imelipa.Katika hali kama hii suala la jamii hii kuihitaji misaada ya kibinadmu ni jambo lililo dhahiri. Katika ziara yangu ambayo nimeitaja hapo juu nilijifunza kwamba  kutoka dunia ya waislamu ni shirika la Uturuki la IHH peke yake ndio linapatikana eneo hilo. Bila shaka misaada zaidi inabidi kuongezwa katika eneo hilo. Waislamu wa Moro katika mchakato wa kupata uhuru wao kamili wanahitaji kwa kiasi kikubwa misaada ya kibinadamu. Ili kuweza kudumu au kuishi kwa muda mrefu wengi wa wanajamii  hii ni watu waliozoea kuishi kwenye migogoro. Hivyo basi mchakato wa kupata serikali huru pia unahitaji kupata msaada wa uzoefu katika kuongoza serikali huru. Msaada pia utahitajika katika maeneo kama mifumo ya kisiasa, mali ya umma, uongozi wa mitaa, shughuli za serikali kuu, elimu ya vyuo vikuu na maeneo mengine kama hayo.Ili juhudi za miaka 500 za waislamu wa Moro zisipotee bure kutokana na kutumia njia ambazo sio sahihi au watu ambao wasio na uwezo, Dunia nzima inapaswa kujitolea kuisaidia Moro.

Vyuo vikuu vikishindwa kuanzisa matawi basi hata vianzishe elimu ya ufundi katika upande wa masuala ya afya na fani nyingine muhimu kwa utawala wa serikali huru kama uongozi wa umma na sheria . hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa.

Umuhimu wa mchango wa Uturuki karika amani ya dunia: Ili kuendesha mazungumzo haya ya amani ya Moro ilianzishwa pia baraza maalum la kimataifa nchini Uturuki. Pamoja na baraza hilo pia ilinzishwa kamati ya uangalizi. Kamati hii ilikuwa na wajumbe 5. Kwa matakwa ya waislamu wa Moro kamati hii ina shirika lisilo la kiserikali nchini Uturuki. Huseyin Oruç ni mmoja wa wajumbe wa kamati hii akiiwakilisha IHH. Kamati ina kazi ya kuangalia mchakato huu wa amani. Hata kama haifahamiki miongoni mwa raia wake, Uturuki kutokana na historia yake, uwezo wake na heshima yake kimataifa ni moja ya nchi ambazo zinaweza kutoa mchango mkubwa katika amani na utulivu duniani.Mchango huu sio serikali peke yake ndio yenye uwezo wa kuutoa, tuchukulie mfano kama ilivyokuwa Ufilipino ambapo mashirika yasiyo ya kiserikali na vyuo vikuu pia yanaweza kuchangia.

Hatua ilipofikia harakati za miaka 500 za Moro ni muhimu sana. Kutoka katika hali ambayo ilikuwa haimfaidishi yeyote mpaka matokeo ya kura ya maoni ambayo yanaleta uhuru na amani kwa waislamu, wafilipino na kwa utu kwa ujumla. Ili watoto wa Moro waweze kuwa na mustakabali ulio salama inabidi kwa pamoja kwa umoja wetu tuchangie katika mchakato huu wa amani.

 

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt.Habari Zinazohusiana