Asilimia 60 ya mapigano ulimwenguni yapo katika mataifa ya kiislamu

Msemaji wa  rais wa Uturuki azungumza  mapigano katika mataifa  ya kiilamu ulimwenguni

Asilimia 60 ya mapigano ulimwenguni yapo katika  mataifa ya  kiislamu

Msemaji wa ikulu mjini Anakara Ibrahim Kalın asema kuwa asilimia 60 ya mapigano na ghasia ulimwenguni yanaendelea katika mataifa ya kiislamu.

Kwa mujibu wa Ibrahim Kalın, mapigano, ghasia na machafuko  ni sababu kubwa  miongoni mwa sababu ambazo zinapelekea athari kubwa  katika jamii.

Mapigano  na ghasia ni  vyanzo vya umaskini na hali duni katika jamii kwa kuwa jamii siokuwa na utulivu ndio jamii ilio  katika hasara kubwa amesema Kalın.

Msemaji wa ikulu ameendelea kusema kwamba  hata liwe na utajiri wa rasili mali kiasi gani, taifa lisilo na uturuli haliwezi hata mara moja kujimudu.

Katika mkutano ulifanyika mjini Ankara Ijumaa katika kituo cha utafiti wa takwimu SESRIC, uchumi,  jamii na mafunzo kwa mataifa ya kiislamu, Kalın amefahamisha kuwa  asilimia 60 za ghasia na  mapigano ulimwenguni ni katika mataifa ya kiislamu.

Hali inayoendelea ulimwenguni katika  karne hii sio tu katika mataifa ya kiislamu amesema Ibrahim Kalın.

Hali hiyo ambayo inaonesha ukosefu wa usalama inashuhudiwa huku na kule ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Kalın, hali iliopo sasa ulimwenguni ni ya kusikitisha kwa  kuwa utajiri uliopo na srasili mal zilizopo zinanufaisha tabaka la watu kadhaa na kulekea maskini kuzidi kuwa maskini zaidi na matajiri kuwa matajiri zaidi.Habari Zinazohusiana