Urusi yawekeza dola bilioni 10 kwenye mradi wa nishati nchini Pakistani

Urusi kupitia shirika lake la Gazprom imetia saini mkataba wa uwekezaji katika nishati nchini Pakistani

Urusi yawekeza dola bilioni 10 kwenye mradi wa nishati nchini Pakistani

Urusi na Pakistani zimeingia makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 10. Katika makubaliano hayo Urusi itapitisha gesi asilia kupitia Pakistani kuelekea Asia ya kusini lakini pia itahusika na utafutaji wa mafuta baharini nchini Pakistani.

Makubaliano hayo yamefikiwa baina ya shirika la kimataifa la mifumo ya gesi la Pakistani (ISGSL) na shirika la Urusi la Gazprom. Utiaji saini wa makubaliano hayo ulifanyika mjini Islamabad na umeshuhudiwa na waziri wa mafuta wa Pakistani Gulam Server Han.

Gazprom,Itahusika na utafutaji wa mafuta baharini nchini Pakistan.

Mradi huo wa bomba la gesi asilia unatajiwa kukamilika ndani ya miaka 4.

 Habari Zinazohusiana