Mogherin ausifu mpango wa INSTEX

INSTEX ni mpango utakaowezeshaUmoja wa Ulaya kufanya biashara na Iran licha ya vikwazo vya Marekani

Mogherin ausifu mpango wa INSTEX

 

Federica Mogherini kiongozi mkuu wa mahusiano ya kimataifa na sera za usalama wa Umoja Ulaya amesema ameupokea kwa furaha mpango wa INSTEX ulioanzishwa na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Mpango wa INSTEX utayawezesha mataifa hayo kufanya biashara na Iran  licha ya vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran.

Mogherini, aliyasema hayo mjini Bucharest ambapo yupo kuhudhuria mkutano wa Gymnich wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama na zinazokusudia kuwa wanachama wa  Umoja wa Ulaya.

Mogherini alisema kwamba siku hiyo mpango wa INSTEX ulianzishwa siku hiyo na utawezesha mataifa hayo kufanya biashara na Iran licha ya vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran.

Marekani imezionya nchi za Umoja wa Ulaya juu ya mpango huo.Habari Zinazohusiana