Aliyozungumza rais Erdoğan baada ya mkutano wake na rais Putin

Haya ndio katika mambo aliyoyazungumza rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan baada ya mkutano wake na rais wa Urusi Vladmir Putin

Aliyozungumza rais Erdoğan baada ya mkutano wake na rais Putin

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan yupo nchini Urusi kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Baada ya mkutano wa ndani na mwenyeji wake rais wa Urusi Vladmir Putin, viongozi hao wakuu wa nchi walikutana na wanahabari. Katika mkutano huo rais Erdoğan alizungumza yafuatayo:

Rais alianza kwa kuzungumzia ajali ya meli iliyotokea mlango bahari wa Kerchi alisema kwamba kati ya waliopoteza maisha wamo raia 4 wa Uturuki akawaombe rehema raia hao na kisha akatuma salamu za rambirambi kwa nchi nyingine zilizopoteza raia wao.

Rais Erdoğan alimshukuru rais Putin pamoja na timu za uokoaji kwa jitihada zao mara baada ya ajali hiyo kutokea.

Rais alisema kwamba kuna ushirikiano mkubwa baina ya Urusi na Uturuki. Kwamba uhusiano wa kiuchumi baina ya mataifa hayo 2 unazidi kuimarika siku hadi siku.

Rais Erdoğan alisema kuna ushirikiano mkubwa baina ya Urusi na Uturuki katika maeneo ya Uchumi, biashara, viwanda, nishati na utamaduni. Na kwamba Utalii ndio umeshika namba moja katika maeneo ya mashirikiano baina ya mataifa hayo.

Rais alisema kwamba thamani ya biashara baina ya mataifa haya mawili imefikia dola za kimarekani bilioni 26. Na kwamba mwaka 2019 utakuwa ni mwaka maalumu. Mwaka huo kutakuwa na shughuli za kiutamaduni na kitalii baina ya mataifa hayo mawili.

Rais pia alisema kwamba mwaka uliopita Uturuki ilipokea watalii karibu milioni 6 kutoka Urusi.

Mwisho rais Erodoğan alizungumzia suala la kuondoa viza baina ya nchi hizo 2 ambapo alisema litakuwa na tija kubwa baina ya raia wa nchi hizo.


Tagi: Uturuki , Urusi

Habari Zinazohusiana