Gharama ya Israel kwa Marekani

Uchambuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazit

Gharama ya Israel kwa Marekani

 

                Siasa za Marekani zinapotazamwa, Hata katika ngazi ya misingi ya siasa hizo kuna maeneo mengi yenye ukakasi. Inaweza kuonekana jinsi siasa hizo zinazingatia zaidi maslahi binafsi.Unapoangalia siasa za Marekani za mashariki ya kati, hata usipoangalia misingi, bado inakuwa ngumu kusema siasa hizi zina faida gani kwa Marekani yenyewe, na wananchi wake.  

Je jamii ya Wamerakani wanafaidikaje kimisingi na kiuchumi na uamuzi wa nchi hio kuwa tofauti na mataifa mengi katika maamuzi ya Umoja wa Mataifa mfano Uamuzi wa Marekani kuitambu Yeruselem kama mji mkuu wa Israel unawafaidishaje wamerekani.

Je kitu gani Marekani ilitaka kukifanya nchini Syria? na nini madhumuni yake? Kuelezea inakuwa ni vigumu.

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimi ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anatufafanulia...

Je ni sawa kwa Marekani kuliunga mkono waziwazi kundi la YPG sehemu ya kundi la PKK laUturuki liliyopo nchini Syria, ukizingatia kwamba Marekani yenyewe inalitambua kundi la PKK kama kundi la kigaidi?

Vitisho kwa Uturuki..

Mara ya mwisho rais wa Marekani alitoa vitisho kwa Uturuki kwamba iwapo italipiga kundi la YPG itawekewa vikwazo vikali vya kiuchumi. Kiuhalisia Uturuki haiogopi vitisho hivyo vya Marekani, na wala haitaweza kuruhusu kuwepo kundi la kigaidi karibu na mipaka yake.

Uturuki haiwezi kuruhusu kundi ambalo kwa miaka 10 limekuwa likiihujumu pamoja  kushumbulia raia wema wasio na hatia lijiimarishe na kuwa taifa huru karibu na mipaka yake.Pamoja na vitisho vya waziwazi vya Marekani lakini kwa kuwa chanzo cha vitisho hivyo ni kundi la kigaidi lililopo katika kanda imebidi Uturuki ishikilie msimamo wake kutofautiana na Marekani kwa hili. Uturuki sio kwamba haina jinsi ya kufanya (haina la kuchagua). Ikibidi Uturuki inaweza kutazama nyanja zote za mahusiano na Marekani na kuanzisha mchakato mpya.

 Katika kujikinga na mchakato au kundi linalotishia amani,usalama na ustawi wake ikihitajika Uturuki inaweza kufanya lolote lile ikiwamo kuvunja mahusiano yote na Marekani hata kama kiuhalisia zipo tahadhari nyingi za kuchukua. Uturuki ya sasa sio ile ya zamani.

 

Je kuna aina yeyote ya busara katika Ujuha wa Marekani mashariki ya kati ?

 Kiuhalisia imefikia mahali ambapo inaweza kusemwa siasa za Marekani mashariki ya kati hazina faida kwa taifa hilo sio kwa misingi wala kiuchumi. Ni aina ya siasa za kijuha.

Kama ilivyokuwa kwa Yerusalem, Je ni kwa nini Marekani ilichukua uamuzi wa kuwa kinyume na mataifa mengine yote ?

Ikifahamu wazi kwamba inaweza kuipoteza Uturuki kimahusiano moja kwa moja, ikumbukwe kwamba Uturuki ni mshirika wa Marekani wa siku nyingi katika NATO na maeneo mengine mengi. Je ni kwa nini Marekani isaliti uhusiano huo na kuliunga mkono kundi la PKK ambalo yenyewe inalitambua kama kundi la kigaidi ?

Ni kwa nini Marekani inatumia lugha inayoashiria mashambulizi ya wazi kabisa dhidi ya waturuki, wakurdi na waarabu wakawaida waliopo mtaani ?

Ni kwa nini iunge mkono waziwazi  kundi ambalo ni la kigaidi ?

Ni kwa nini Marekani iyafanya yote haya ?

 

Sababu ni Israel

Kwa mujibu wa Marekani yenyewe, inayafanya haya yote kwa lengo kuikomesha Daesh na Iran. Lakini majibu hayo ya Marekani hayaingii akilini hata kidogo.

Unapozitazma siasa zisizotabirika za kijuha za Marekani, Katika kanda hii hasa katika masuala yanayohusiana na Israel inaonekana jinsi gani kwa namna fulani Marekani inavyoshikiwa akili. Kwa sababu Marekani katika masuala yanayohusiana na Israel hata maslahi yake binafsi huwa inayaweka pembeni. Linapokuja suala la Israel bila shaka Marekani imekuwa ikitumia siasa za kijuha. Hili linaleta hasara kubwa kwa Marekani yenyewe, Israel pamoja na kwa wayahudi wasio wazayuni.

Gharama ya Israel kwa Marekani:

Maslahı ya Marekanı hayazıngatıwı: Katika zama hizi tunazoishi mara nyingi siasa za nje za nchi hujengwa kwa misingi ya kuifaidisha nchi husika. Linapokuja suala Israel Marekani hutoa kafara hata maslahi yake binafsi.Huwa kinyume na haki,uhuru, haki za binadamu na maadili mengine kama hayo ya kijumla: Huunga mkono siasa za ukandamizaji na mabavu za Israel bila masharti yeyote. Kiuhalisia dunia nzima inalaani tabia hii ya Marekani.Na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo upinzani dhidi ya Marekani unavyoongezeka.

Kwenda kinyume na nchi na wananchi wa kanda: Kwa Marekani kufuata siasa za kijuha zinazoitazama Israel peke yake katika kanda hii, Kutumia lugha inayoashiria hatari kwa mataifa mengine ya kanda. Hata kama mataifa yatalikalia kimya suala hili,watakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa jamii.

Kwa siasa za Nje za Marekani linapokuja suala linalohusu Israel, inapoteza uhuru wake.

Kuifanya Israel kuwa na kiburi zaidi: Kitendo cha Marekani kuiunga mkono Israel kijuha, bila kutumia akili, kunaipa kiburi zaidi Israel na kuifanya iendeleze siasa zake za kibabe na kiunevu. Kuongezeka kwa ubaguzi dhidi ya wayahudi: Uungaji mkono inaoutoa Marekani kwa Israel bila masharti yeyote kunakopelekea kiburi na ubabe wa Israel kuongezeka. Na kutokana na vitendo vya uonevu vinavyotelezwa na Israel imepelekea chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi kuongezeka duniani. Ingawa ni ukweli usiofichika kwamba ubaguzi ni jambo lisilokubalika bila kuzingatia ubaguzi huo unafanywa na nani dhidi ya nani.

 Kuongezeka kwa Hatari katika usalama wa Israel: Uungaji mkono wa Marekani kwa Israel usiokuwa na masharti kimsingi hauisaidii Israel katika upande wa Usalama. Ni aina ya siasa ambayo inaongeza wasiwasi katika suala la usalama. Israel isiyo ya kibabe yenye kufuata siasa za kirafiki zisizo na dhulma ndiyo itakuwa suluhisho kwa upinzani dhidi ya Israel.

 Kwa nini Marekani inaunga mkono kiasi hichi Israel bila kikwazo au masharti yeyote Ingawa leo au kesho inaweza kuipoteza Israel ? hilo nalo ni suala tofauti linalohitaji makala yake. Kwa leo turidhike kwamba sio kila mtu nchini Marekani anaunga mkono siasa hizi za kijuha zinazofanywa na Marekani, Nchi yenye nguvu kama zote duniani kushikwa akili na nchi ndogo.

 

Uchambuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım BeyazitHabari Zinazohusiana