Kazi za TIKA sehemu ya pili

TIKA imeanzisha mbinu mpya ya aina ya Kituruki ya misaada ya maendeleo

Kazi za TIKA sehemu ya pili

Ikiwa ni wiki ya pili tunazungumzia kuhusu wakala wa ushirikiano na maendeleo Uturuki, TİKA.Wiki hii tutaendele kuangalia kazi za shirika la TİKA .

Kufikia hivi leo TİKA imeweza kutekeleza miradi 4,250 ya elimu ikiwamo elimu ya ufundi katika mataifa mbalimbali yakiwemo Kolombia, Palestina,Nijer,Masedonia,Albania,Afghanstan n.k shirika hili pia kwa kuanzisha taasisi mpya za kielimu, katika miaka 5 ya hivi karibuni shirika limejenga na kukarabati zaidi ya shule 1000 katika nchi mbalimbali.  

TİKA,inatekeleza miradi mbalimbali katika fikra ya kupunguza umaskini,kuleta maendeleo vijijini pamoja na kutoa ajira kwa wanawake vilevile shirika hilo linaweka kipaumbele katika kuhakikisha kunakuwako na usalama wa chakula pamoja na kuchangia katika shughuli za kuleta kipato katika kaya masikini. TIKA inatekeleza miradi mbalimbali katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Katika kupambana na ukame barani Afrika na kuhakikisha rasilimali na utajiri uliokuwamo barani humo unazinufaisha jamii za wazawa wa bara hilo. 

TIKA imeanzisha shule ya mfano mjini Mogadishu nchini Somalia ambayo itahudumia kanda yote. Shule hiyo inafundisha mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa. Katika nchi za Balkan  pia TIKA ina miradi mingi ya muda mrefu katika nyanja ya kilimo cha kisasa, hayo yote yamesaidia kaya masikini kujiongezea kipato.

Kipaumbele chingine cha TİKA ni kutoa elimu za ufundi katika fani mbalimbali na kuanzisha taasisi za kiufundi. TIKA imenzisha kiwanda cha kiwanda cha kutengeneza mafuta ya Zeytun mjini Gaza, kiwanda hicho kinaitwa kiwanda cha mafuta ya zeytun cha Abasan. Mradi huu ni mradi wa mfano katika kanda katika kutengeneza ajira pamoja na kukuza uchumi.Mwaka 2017 Kiwanda hicho kiliweza kuwanufaisha wakulima 3,100 kwa kununua mazao na huduma zao. Mwaka 2016 kiwanda hicho kiliweza kuzalisha tani zipatazo 5,000 za mafuta ya Zeytun. Kila tani moja iliyozlishwa iliingizia serikali ya mji wa Abasan dola za kimarekani 100.

 

Mbinu mpya: Aina ya Kituruki ya misaada ya maendeleo

TİKA, imeanzisha mbinu mpya ya aina ya kituruki ya misaada ya maendeleo. Mbinu hiyo ina misingi ifuatayo:   

              Kutokuwa na  masharti                                   Kutoa kwa moyo mkunjufu

Uwazi

Kuwalenga watu

Kuwajibika kwa pamoja

Kujifunza kwa pamoja

Kuzingatia mahitaji

Kuzingatia masulihisho ya matatizo


Tagi: TIKA

Habari Zinazohusiana