Sateliti mpya ya Iran

Aliyoyasema rais wa Iran Hasan Ruhani kuhusu Sateliti mpya ya nchi hiyo

Sateliti mpya ya Iran

 

Kutokana na kushindwa kwa jaribio la hivi karibuni, Iran inajiaanda kurusha sateliti nyingine.

Rais wa Iran Hasan Ruhani amesema suala la utengezaji wa sateliti na urushaji wa sateliti hizo angani ni muhimu sana kwa taifa hilo na katika miezi ijayo wanajiandaa kurusha sateliti nyingine angani.

Ruhani, akiongea  mjini  Tehran katika mkutano na mawaziri alisema hata kama hawakufanikiwa inavyotakikana bado wamepiga hatua kubwa katika suala zima la utengenezaji na urushaji wa sateliti. Hayo aliyasema katika mkutano wa mawaziri uliofanyika mjini Tehran wakati akizungumzia kuhusu jaribio walilolifanya siku ya Jumapili la kurusha sateliti waliyoiita  "Peyam". Sateliti hiyo haikufanikiwa kufikia hatua ya kukaa kwenye njia yake angani "obit". 

Mnamo Januari 3,waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo aliitolea onyo Iran kuachana na mpango wake wa kutengeneza roketi za aina zote, zikiwemo za kurushia sateliti hizo.

Waziri wa Habari na teknolojia ya mawasiliano wa Iran Muhammed Cevad Azeri Cehromi, alitangaza kwamba hivi karibuni watairusha sateliti yao iliyotengenezwa nchini humo inayoitwa "Dusti" ikimaanisha urafiki.

 


Tagi: Iran , Sateliti

Habari Zinazohusiana