Maandamano ya kupinga uislamu nchini Uholanzi

Maandamano dhidi ya uislamu mbele ya mskiti Abi Bakr Issıdik  Uholanzi

Maandamano ya kupinga uislamu nchini Uholanzi

Wafuasi wa chama cha mrengo wa kulia Pegina nchini Uholanzi wameandamana mbele ya mskiti wa Abi Bakr Issidik  Utrecht kupinga uislamu.

Maandamano hayo yamefanyika Jumatato dhidi ya waislamu.

Ifahamike kwamba  mskiti wa Utrecht ni mskiti ambao waumini wake wengi ni raia wenye  asili ya  kigeni  wengi wao wakiwa ni raia kutoka nchini Morocco.

Katika maandamano hayo, waandamanaji wa Pegina walikuwa na mabango yalioandikwa maneno ya kashfa dhidi ya uislamu na  kuonesha filamu  ambayo inakashifu uislamu.

Jeshi la Polisi limeimarisha usalama pembezoni mwa msikiti huo kuzuia ghasia kutokea.

Ghasia ziliibuka kati ya jeshi la Polisi na waandamanaji wa Pegina huku watu wawili wakiripotiwa kukamatwa.

Muhusika wa upashaji habari katika mskiti huo Jamal Huri  ameliambia shirika la Anadolu kuwa kitendohicho ni  uchokozi.Habari Zinazohusiana