Alichosema Rais Erdoğan kuhusu shambulizi la Manbij

Hiki ndicho alichokisema rais Erdoğan kuhusu shambulizi la Manbij lillilopelekea vifo vya watu 20 wakiwemo wanajeshi 5 wa Marekani

Alichosema Rais Erdoğan kuhusu shambulizi la Manbij

Rais wa Marekani Recep Tayyip Erdoğan, amesema anafahamu katika shambulizi la kigaidi lililofanyika Manbij nchini Syria watu 20 waliuawa ikiwemo wanajeshi 5 wa Marekani.

Erdoğan,aliyasema hayo katika mkutano wa pamoja na wanahabari baina yake na rais wa Croatia, Kolinda Grabar Kitarovich ambaye yupo Ankara kwa ziara rasmi ya kikazi. Rais Erdoğan alisema shambulizi hilo la Manbij inawezekana linalengo la kuathiri uamuzi wa Marekani kuondoa majeshi yake nchini Syria.

Erdoğan, alisema kwa hesabu za magaidi shambulizi hilo zitamfanya rais Donald Trump afikirie mara mbili na pengine aufute mpango wa kuondoka Syria, na ikitokea imekuwa hivyo inamaanisha Daesh watakuwa wamefanikiwa wanachokitaka.

Rais Erdoğan, alisema Uturuki itaendeleza vita dhidi ya Daesh kuhakikisha wanalimaliza kundi hilo la kigaidi katika ardhi ya Syria. 


Tagi: Erdoğan

Habari Zinazohusiana