Maduro aapishwa nchini Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameapishwa katika mhula wa pili nchini Venezuela.

Maduro aapishwa nchini Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameapishwa katika mhula wa pili nchini Venezuela.

Sherehe ya kuchukua kiapo imefanyika katika mji mkuu wa Caracas baada ya Maduro kuchaguliwa kwa mara nyingine Mei iliyopita.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 56 aliingia madarakani mwaka 2013 baada ya kiongozi aliyekuwa madarakani Hugo Chavez kupoteza maisha.

Maduro amechaguliwa kutawala kwa miaka sita mingine.

Makamu wa rais wa Uturuki Fuat Oktay, ambaye aliwasili mji mkuu wa Venezuela mwishoni mwa Jumatano na kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais huyo.

Wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 90, ikiwa ni pamoja na Rais wa Bolivia Eva Morales na Rais wa Cuba Miguel Mario Diaz-Canel, wamehudhuria sherehe hiyo.

Wakati huo huo, kundi la Lima, ambalo linahusu nchi nyingi za Amerika ya Kusini, walisema kuwa hawatambui urais wa Maduro.

 

 Habari Zinazohusiana